'ACTION AUTO GARAGE' YAFUNGULIWA DODOMA.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Leo Agosti 15/2024, amezindua karakana ya kisasa ya Toyota ( Action auto Garage) inayojihusisha na utengenezaji wa kisasa wa magari inayopatikana Nzuguni Jijini Dodoma. Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Senyamule amewataka madereva wa magari kupatiwa Elimu Ili kuepusha uharibifu na kuzuia uchakavu wa vyombo hivyo unaotokana na Uzembe. "Mkurugenzi wa Garage hii amesema madereva wanatakiwa waje wapate Elimu, kwa hiyo nisisitize jambo hili Kwa Taasisi zote za Serikali na watu Binafsi, Magari haya yana gharama kubwa sana kwa hiyo tunategemea yakae muda mrefu lakini ukiona yamekaa muda mchache ujue kuna tatizo mahali na matatizo mengi unakuta si ya mtengenezaji ila ni ya kwetu kwa sababu ya kutofuata maelekezo ya matumizi husika ikiwemo kufanya Service Kwa wakati kwa hiyo inatakiwa upatiwe Elimu ya kutosha", Mhe. Senyamule Aidha Mhe. Senyamule amewapongeza Toyota Tanzania Kwa kufungua Chumba Cha maonesho ya magari Mko...