Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiongozana na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu na Mkurugenzi wa Jiji Bw. Joseph Mafuru leo Mei 11, 2023 wamepokea ugeni kutoka China ukiongozwa na Bw. HuaRong Zhang mmiliki wa Huajian group akiwa na lengo la kuwekeza katika Kiwanda kikubwa cha Kutengeneza viatu.

Mhe. Senyamule amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za uwekezaji nchi na amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.

Comments