Posts

Showing posts from March, 2024

WANAFUNZI WAASWA KUZINGATIA NIDHAMU SHULENI.

Image
Juma la wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma limetamatika Kwa viongozi mbalimbali  wa Mkoa wa Dodoma kuzungumza na kushiriki Chakula Cha Mchana na wanafunzi wa Shule za kidato Cha Sita za Mkoa huo. Kwa nyakati tofauti akiwa katika shule ya Sekondari ya wavulana Kongwa na Shule ya wasichana kibaigwa amewaasa wanafunzi hao wa kidato Cha sita kuendelea kudumisha nidhamu hususani katika kipindi hiki wanachojiandaa na mitihani Yao na kuachana na marafiki wasiofaa ambao watawasababishia matokeo yatakayogharimu maisha ya ndoto zao. "Tunataka A zenye nidhamu, hapa Kuna wenzenu wamechafua jina la Shule na nyie mliopo hapa tunategemea nyie mtabadilisha sura hii ambayo sio njema Kwa Mkoa, acheni tabia ya kufata mkumbo Kwa kushawishiana mambo yasiyofaa kwasababu Kila mtu ana ndoto zake na Kila moja atarudi nyumbani kwao kivyake na usipokuwa makini utaharibu maisha yako Kwa mikono yako mwenyewe kwasababu tuu ya ushawishi usiofaa kutoka Kwa marafiki zenu. "Lazima muamue kuachana na baadhi ya mamb...

VIJANA WA SKAUTI WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI KATIKA MAENEO YAO

Image
Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya juma la Elimu Mkoa wa Dodoma Leo Machi 21,2024 Afisa Vijana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw.Tumsifu Mwasamale amefunga mafunzo ya wahitimu 30 wa Skauti  kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa huo ikiwa ni  moja ya mkakati wa Mkoa wa kuendeleza mafunzo hayo  katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Don Bosco Jijini Dodoma. Akizungumza na wahitimu hao Bw. Mwasamale amewataka kuhakikisha wanakuwa chachu kwa wengine katika Halmashauri zao kwa kuonesha weledi waliojifunza ili kupunguza mmomonyoko wa maadili miongoni mwao.  Kilele cha juma la Elimu lililoanza tarehe 18 Machi, 2024 kinatarajiwa kutamatika tarehe 25 Machi,2024 ambapo kauli mbiu ni "Uwajibikaji wangu,ndio Msingi wa kuinua ubora wa Elimu na Ufalu Dodoma".
Image
  Wawakilishi wa Shirika la World Food Program (WFP) Tanzania wakiongozwa na Bi. Sarah Gordon Gibson, leo March 18,2024 wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa lengo la Kuutambulisha mradi wa maboresho ya Tehama katika Soko la Kibaigwa Wilayani Kongwa. Mradi huo wenye lengo la kuimarisha miundombinu ya mawasiliano katika soko hilo unatarajiwa kuanza Mwezi April na kukamilika mwezi Juni mwaka huu na unatarajia kugharimu zaidi ya Dollar za kimarekani elfu hamsini, ambapo fedha hizo zitatolewa na shirika hilo.

MCHAKA MCHAKA HUIMARISHA AFYA NA UZALENDO

Image
Wakuu wa Shule za msingi Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kuweka utaratibu kwa wanafunzi kukimbia mchaka mchaka asubuhi kabla ya masomo kwani zoezi hili lina faida nyingi ikiwemo kuimarisha afya ya akili, ukakamavu pamoja na uzalendo kupitia nyimbo zinazoimbwa wakati wa zoezi hilo. Hayo yamebainishwa leo Machi 19, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa uzinduzi wa Juma la wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Dodoma iliyopo Jijini humo. "Kupitia Juma hili, tutadhihirisha Dodoma tumeamua kufanya Mapinduzi kwenye Elimu. Nitoe maelekezo hapa, shule zote ziweke utaratibu kwa wanafunzi kukimbia mchaka mchaka kwani zoezi hili lina faida kubwa kwao kama vile kuimarisha afya ya akili, ukakamavu kupitia kukimbia pamoja na uzalendo kutoka na zile nyimbo zinazoimbwa" Amesema Mhe. Senyamule Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amezungumzia umuhimu wa michezo kwani Juma hili linakwenda sambamba na Bonanza la michezo mbalimbali kuelek...