Wawakilishi wa Shirika la World Food Program (WFP) Tanzania wakiongozwa na Bi. Sarah Gordon Gibson, leo March 18,2024 wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa lengo la Kuutambulisha mradi wa maboresho ya Tehama katika Soko la Kibaigwa Wilayani Kongwa.
Mradi huo wenye lengo la kuimarisha miundombinu ya mawasiliano katika soko hilo unatarajiwa kuanza Mwezi April na kukamilika mwezi Juni mwaka huu na unatarajia kugharimu zaidi ya Dollar za kimarekani elfu hamsini, ambapo fedha hizo zitatolewa na shirika hilo.
Comments
Post a Comment