VIJANA WA SKAUTI WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI KATIKA MAENEO YAO















Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya juma la Elimu Mkoa wa Dodoma Leo Machi 21,2024 Afisa Vijana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw.Tumsifu Mwasamale amefunga mafunzo ya wahitimu 30 wa Skauti  kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa huo ikiwa ni  moja ya mkakati wa Mkoa wa kuendeleza mafunzo hayo  katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Don Bosco Jijini Dodoma.

Akizungumza na wahitimu hao Bw. Mwasamale amewataka kuhakikisha wanakuwa chachu kwa wengine katika Halmashauri zao kwa kuonesha weledi waliojifunza ili kupunguza mmomonyoko wa maadili miongoni mwao. 

Kilele cha juma la Elimu lililoanza tarehe 18 Machi, 2024 kinatarajiwa kutamatika tarehe 25 Machi,2024 ambapo kauli mbiu ni "Uwajibikaji wangu,ndio Msingi wa kuinua ubora wa Elimu na Ufalu Dodoma".

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA