DCT NA NEEMA YA MILLIONI 32.8 MWITIKILA-BAHI

Vifaa vya Shule vyenye thamani ya Tsh.Millioni 32.8 vimekabidhiwa katika Shule za Msingi Mwitikira, Lupeta Mwitikira B na Shule ya Sekondari Mwitikira kwa ufadhili wa Kanisa la St. Pauls Richmond kutoka Marekani kwa kushirikiana na kanisa la Anglican Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), ambapo makabidhiano hayo yamefanyika April 17, 2024 katika viwanja vya kanisa la Anglican Parish ya Mwitikila Wilayani Bahi. Vifaa hivyo ni madawati 290, meza 13, Viti 113 na Mashine ya kuchapia na kutolea kopi (printer machine) vimekabidhiwa na Askofu wa DCT Dickson Daud Chilongani kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mayeka S. Mayeka ambaye amewakabidhi uongozi wa Halmashauri ya Bahi na Uongozi wa Shule hizo. Akizungumza katika Hafla hiyo Mhe.Mayeka amewataka wakazi wa kata ya Mwitikira kuacha tabia ya kuwaachisha Watoto wao shule na kuwapeleka katika majiji mbalimbali kwa lengo la kufanya kazi za ndani zisizo na maslahi katika Maisha ya Watoto hao. “Kuna mawakala wanaobeba Watoto vijijin...