Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma Kwa kushirikiana na Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) wameandaa Iftar iliyowajumuisha watoto wenye Mahitaji maalum, walemavu, wazee na wajane iliyofanyika Leo April 7 katika bwalo la Shule ya Sekondari Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki hafla hiyo ambapo amewapongeza wanawake hao kwa kuikumbuka jamii inayowazunguka hususani katika kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Aidha Mhe. Senyamule amewataka wajane hao kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotelewa na serikali kwani serikali inatambua na kuthamini uwepo wao ikiwemo kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri zao na kufanya biashara ambazo zitawasaidia kukidhi mahitaji yao.
Hata hivyo Senyamule ametumia fursa hiyo kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wahitaji, wajane na wazee waliofika kushiriki Iftar hiyo.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment