VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
Viongozi wa soko la wazi la Machinga lililopo Mtaa wa Kitenge, Kata ya Majengo katika Jiji la Dodoma, wamesimamishwa uongozi kupisha uchunguzi kutokana na kudaiwa kutenda makosa ya kiuongozi na kijinai kwa wafanyabiashara wa soko hilo. Agizo hilo limetolewa Septemba 13, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule alipokua akitatua kero za wafanyabiashara wa soko hilo katika Mkutano wa hadhara aliouitisha ndani ya soko hilo. Wafanyabiashara hao, walipata fursa ya kutoa kero zao mbele ya Kiongozi huyo lakini kubwa zaidi ni lawama walizotupiwa viongozi wa soko ambao ni Mwenyekiti na Meneja kwa kuuza vizumba kinyume na taratibu pia kughushi barua za Mkurungenzi wa Jiji pamoja na vitambulisho vya wajasiriamali. "Zipo tuhuma za kiuongozi lakini nyingine za jinai kama kufoji vitambulisho na barua. Hatuna uhakika mpaka uchunguzi ufanyike. Wakati uchunguzi unafanyika Mwenyekiti na Meneja wasimamishwe kwani wameonekana katika sehemu kubwa ni sehemu ya tatizo." Ameagiza Mh...