DODOMA YAWEKA MIKAKATI KUMALIZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.

Mkoa  wa Dodoma umejipanga  kufikia mwishoni mwa mwaka huu kuwa na  vituo 60 vinavyotoa huduma za dharura za upasuaji kwa kina mama wajawazito wenye viashiria vya hatari.


Hayo yamebainishwa leo Septemba 09, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Simon Mayeka, wakati wa mkutano wa tathimini ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji huduma za  afya ya uzazi na mtoto chini ya ufadhili wa Shirika la KOFIH unaotekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Mkoa wa Dodoma una jumla ya vituo vya afya 546 vikijumuisha hospitali 17, vituo vya afya 68, zahanati  431 na kliniki 30.

Aidha vituo 416 sawa na asilimia 76 vinatoa huduma za afya  ya uzazi na mtoto na vituo 48 sawa na asilimia 56 kati ya vituo 85 vinatoa huduma za dharura  za upasuaji kwa kina mama wajawazito.

“Mkoa umejipanga kuongeza vituo hivyo ili kufikia vituo 60 ifikapo Desemba 2024, huduma za dharura za upasuaji kwa kiina mama wajawazito wenye viashiria vya hatari zimeendelea kuboreshwa ambapo hadi sasa Mkoa una jumla ya vituo 48,” alisema

Ameongeza kuwa, vituo 44 vipo ngazi ya msingi (vituo vya afya ,hospitali za halmashauri) ambapo hilo ni ongezeko kubwa kwani mwaka 2020 kulikuwa na vituo 29 vinavyotoa huduma ya upasuaji ukilinganisha na vituo 48 mwaka 2024.

Aidha, taarifa ya utafiti uliofanyika mwaka 2020 ya viashiria vya huduma za afya ya uzazi, Mkoa wa Dodoma ulionekana kufanya vizuiri ukilinganisha na takwimu za kitaifa.

Baadhi ya matokeo ya viashiria hivyo ni kina mama wajawazito waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya kitaifa ilikuwa asilimia 81 na kwa Mkoa wa Dodoma ilikuwa ni asilimia 90.0

Pia kina mama waliozalishwa na watoa huduma wenye ujuzi kitaifa ilikuwa 84.8% huku Mkoa wa Dodoma ilikuwa 93.2%, kina mama wajawazito waliohudhuria kliniki mahudhurio manne au zaidi kitaifa ilikuwa 65% na kwa Mkoa wa Dodoma ilikua 76.8%

Pamoja na hayo alisema mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano ambapo ulianza 2021 na unatarajia kukamalika mwaka 2025 ambapo unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Kongwa na Mpwapwa na unatarajiwa kutumia kiasi cha dola Milioni 4.2

Kadhalika, katika kipindi cha miaka mitatu (2021-2023) ya utekelezaji wa mradi, kiasi cha fedha za kitanzania Sh 2,727,017,476.43 zimetumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Afisa programu uzazi salama Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto, Bw. Fideo Obimbo, ameshukuru utekelezaji wa Mradi huo.

“Mradi huu unakwenda sambamba na jitihada za Serikali kupunguza vifo vya mama na mtoto ili kufikia malengo ya Milenia ifikapo 2030. Hadi sasa vifo vitokanvyo na uzazi Pamoja na Watoto wachanga vimepungua hadi vifo 76 kati ya vizazi hai 100,000 hivyo mradi huu utakwenda kusaidia kupunguza vifo hivi" Bw. Obimbo

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA