OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA YAFANYA MKUTANO WA KUMSHUKURU NA KUMPONGEZA RAIS,MHE. SAMIA SULUHU HASSAN
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo imefanya mkutano wenye lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa PSSSF ambapo watumishi wa sekta mbalimbali za Serikali katika mkoa wa Dodoma walihudhuria. Akifungua mkutano huo, Katibu Tawala Mkoa Dkt Fatma Mganga, alianza kwa kupongeza jitihada za Rais Samia suluhu Hassan hasa kwenye ongezeko la mishahara pamoja na posho. Dkt. Mganga amewataarifu wajumbe wa mkutano huo kuwa Mkoa wa Dodoma una watumishi zaidi ya Elfu 20, hivyo ongezeko hilo litaleta afueni kwa kugusa familia zaidi ya hizo. Katika kutoa pongezi na shukrani hizo, watumishi wa idara mbalimbali wakiwakilishwa na wasemaji wao,ambapo wengi wao wamempongeza Rais kwa kuwajali na kuwakumbuka katika ongezeko hilo kwani litakua chachu ya kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuinua uchumi wa familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla. Akizungumza kwa niaba ya Walimu, mwenyekiti wa C...