OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA YAFANYA MKUTANO WA KUMSHUKURU NA KUMPONGEZA RAIS,MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo imefanya mkutano wenye lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa PSSSF ambapo watumishi wa sekta mbalimbali za Serikali katika mkoa wa Dodoma walihudhuria. 

Akifungua mkutano huo, Katibu Tawala Mkoa Dkt Fatma Mganga, alianza kwa kupongeza jitihada za Rais Samia suluhu Hassan hasa kwenye ongezeko la mishahara pamoja na posho. Dkt. Mganga amewataarifu wajumbe wa mkutano huo kuwa Mkoa wa Dodoma una watumishi zaidi ya Elfu 20, hivyo ongezeko hilo litaleta afueni kwa kugusa familia zaidi ya hizo. 

Katika kutoa pongezi na shukrani hizo, watumishi wa idara mbalimbali wakiwakilishwa na wasemaji wao,ambapo wengi wao wamempongeza Rais kwa kuwajali na kuwakumbuka katika ongezeko hilo kwani litakua chachu ya kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuinua uchumi wa familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla. 

Akizungumza kwa niaba ya Walimu, mwenyekiti wa Cha Walimu Mwalimu Samwel Malecela amempongeza Rais kwa kuwapandisha madaraja walimu zaidi ya 2300. Aidha walimu wamefarijika sana kwa punguzo la 6% ya mikopo ya Elimu ya juu,na ongezeko la umri wa wategemezi katika bima ya afya kutoka miaka 18 hadi miaka 21.

Akizungumza mwakalishi wa Wauguzi , ameeleza kuwa ongezeko la mishahara na posho limeleta motisha ya hali ya juu na kuwafanya wafanye kazi kwa moyo mmoja. 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, aliishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiangalia kwa karibu sekta ya miundombinu hasa kwa mkoa wa Dodoma ambao ndio makao makuu ya nchi. Mhe. Shekimweli ameongeza kuwa Serikali imeanzisha miradi mbalimbali ndani ya Mkoa ikiwemo ujenzi wa Uwanja mkubwa wa ndege wa Msalato, miradi ya Barabara za mizunguko, ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR hivyo Mkoa unatakiwa kuisimamia kwa karibu miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati kwani faida yake si kwa mkoa tu bali kwa Taifa zima. Mbali na miradi ya ujenzi wa miundombinu, pia ndugu Shekimweri ameishukuru Serikali kwa kuondoa makato ya asilimia 6 kwa wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu, ongezeko la posho kwa watumishi na ongezeko la pensheni kutoka asilimia 25 hadi 33 na amewataka watumishi wote kila mmoja kuweka dhamira ya kuhakikisha maboresho hayo yanaleta mabadiliko kwenye utendaji kazi na hata kwenye familia zao. 

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Joseph Mafuru amesema kuwa Jiji la Dodoma lina watumishi takribani 4,057 ambao wanaguswa na ongezeko la mishahara na posho hivyo imeongeza morali ya kufanya kazi na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.Mkurugenzi amewataka watumishi waanze kufanya uwekezaji ili kufungua uchumi wa ndani kwani Halmashauri inaendelea kusimamia miradi mbalimbali iliyoanzishwa ikiwemo ujenzi wa Jengo litakalotumiwa na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Soko la Machinga ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7. Mhe. Rais Samia ameongeza kiasi cha Bilioni 2.5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo. 

Mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi nchini Ndugu Wandiba alipata fursa ya kumshukuru Rais Samia kwa ongezeko hilo na kusema kuwa wafanyakazi wamefurahi sana kwani wamewazidi hata nchi jirani ya Kenya ambako ongezeko la mshahara ni la asilimia 14 wakati Tanzania ni asilimia 23.3.Hii inaonyesha kuwa Rais amefanya usikivu wa hali ya juu pindi wafanyakazi walipowakilishwa kutoa mapendekezo yao juu ya ongezeko la mishahara kwani ndio ilikua kiu yao.

 Akizungumza Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Mwamfupe katika kuonyesha shukrani za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wote wa Umma katika Dodoma kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa na hivyo na kutoa utumishi uliotukuka kwa kila mgeni atakayetembelea mkoa wa Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka ambaye ndiye ameandaa Kongamano hili kwa kushirikiana na ofisi yake, alihitimisha kwa kusema kuwa lengo la mkutano huo ni kumshukuru na kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kwa nchi na hasa kwa hatua zake za kuboresha maslai ya Watumishi waUmma hapa nchini. Maboresho haya yameongeza morali na ari ya ufanyaji kazi,hivyo tukiwa Watumishi wa Umma morali hii ni vyema iendane na matokeo na tuibebe morali hii moyoni. “Karne ya 21, utumishi wa Umma inabidi uendane na ubunifu.Tunapoenda kwenye miradi mipya ni vyema miradi hiyo ikaendana na ubunifu. Malipo ya malimbikizo yalete mabadiliko katika maisha yetu.Tusiweke heshima Bar, badala yake tuweke heshima nyumbani. Katika Halmashauri zetu tufanye vitu ambavyo vitaonyesha kwamba kwa tunamshukuru Mhe.Rais. Nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3, nyongeza ya posho na nyongeza ya kikokotoo toka 25% hadi 33% zituhamasishe tufanye kazi zenye matokeo”. Amesisitiza Rc. Mtaka.

 Aidha Mhe.Mtaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani kwa kupata tuzo ya heshima ya BABACAR NDIAYE (2022), Accra Ghana.Mwisho. 





























Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA