Kwa Pamoja Tunaweza _ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma
Katika kujenga Umoja, ushirikiano na kujengeana uwezo katika Masuala mbalimbali ya kiofisi na kijamii. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma iliamua kuja na utaratibu wa Chakula cha Pamoja kila jumatano ya mwisho wa mwezi. Katika Jumatano hiyo Taasisi mbalimbali hukaribishwa kuja kutoa mada na kuwaeleimisha wafanyakazi wa mkoa kuhusu masuala mbalimbali.Sanjari na hayo chakula hicho cha mchana hutumika kuwapongea wafanyakazi wote waliozaliwa katika mwezi husika . Katika Chakula cha mchana kilichofanyika 27/7/2022 Bpodi ya maziw ilikaribishwa kutoa mada na kuwahamasisha Watumishi kuhusu matumizi bora ya maziwa kuliko kimiminika kingine ,kwani kila binadamu anatakaiwa kunywa nagalau lita 200 mza maziwa kwa mwaka. Mwisho Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waliozaliwa mwezi wa Julai wakifungua Champagne Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma waliozaliwa mwezi Julai Wakikata keti kwa pamoja Watumishi wa Bodi ya Maziwa wakionyesha bidhaa zao