"Machinga Complex -Dodoma. Mfano wa Kuigwa "- Mhe. Seleman Jafo
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea Soko la Machinga Complex lililopo jijini Dodoma. Mhe. Jafo amesema kuwa pamoja na kutembelea soko nimekuja kuona kama mambo ya mazingira yamezingatiwa katika Ujenzi wa Soko hili la Machinga Complex.
“Hii ni pamoja na kuangalia mambo makubwa matatu, kuangalia
matumizi ya nishati,maana nimesikia kutakuwa na wamachinga ambao watakuwa
wanapika vyakula hivyo nimekuja kuona
kama watatumia nshati ya aina gani kama kuni au mkaa au gesi, pia
nimekuja kuona mfumo wa maji safi na maji taka, pamoja na mfumo wa
kuhifadhi maji ya mvua. Aidha nimekuja
kuona jinsi ambavyo mtahifadhi taka maana Wizara yangu inashughulika na mambo
yote hayo “ Amesema Mhe. Jafo.
Akielezea hali ya ujenzi wa Soko hilo ambao umezingatia
mazingira kwa kiasi kikubwa, Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw.Dickson Kimaro
amemshukuru Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira kwa
kutembelea eneo hilo na kumhakikishia
kuwa ujenzi wa soko hilo umezingatia masuala yote ya kujali mazingira
kwani Wapishi hawatatumia kuni wala mkaa
badala yake watatumia gesi na tayari kuna sehemu maalumu za kuhifadhia mitungi ya gesi hizo.
Kuhusu suala la mfumo wa maji taka, bwana Kimaro
amemhakikishia Mhe. Jafo kuwa tayari
kuna mfumo wa maji safi na maji taka
na kuwa wanafanya kazi kwa
ukaribu sana na DUWASA. Aidha kuna maeneo matatu ya kuchomea taka, kuna eneo la kuchomea taka ngumu,eneo la taka za
chupa na eneo la taka za karatasi na
chakula. Maeneo yote haya yatatumika kuhifadhia taka kabla ya kupelekwa Dampo.
Pamoja na hayo Kaimu Mkurugenzi amemhakikishia Mhe. Jafo kuwa Soko limezingatia
mfumo mzuri wa kuhifadhia maji ya mvua
ambapo maji ya mvua yatakuwa yanakusanywa na kuhifadhiwa kwenye
tenki la lita 150,000.
Nae Mkandarasi Bw.
Taher Mustafa, ameonyesha kufurahishwa na ziara ya Mhe. Jafo kwani ziara za
viongozi zimekuwa kichocheo kwao kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Bw.Mustafa
ameeleza kuwa mafaniko makubwa katika kazi yao yamesabishwa na usimamizi
madhubuti wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
pamoja na Timu yake.
Aidha mara baada ya kupokea maelezo ya Kaimu Mkurugenzi na
Mkandarasi Mhe. Jafo alitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
Kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,ili
asaidie upatikanaji wa natural gesi moja kwa moja. “Wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC ili
waje kuweka mtungi mmoja ambao watu watakuwa wanalipia. Soko hili ni la kisasa na la mfano Tanzania, hivyo watu
watafungiwa meter na kuanza kulipia gesi
kulingana na matumizi”.Amesisitiza Mhe.
Jafo.
Mhe Jafo amepongeza uwepo wa udhibiti madhubuti wa
maji," Cha muhumi haya maji ya mvua yakijaa kwenye tank badala ya kuanza
kufurika humu ndani basi kuwe na njia ya
kuyatoa nje. Pia ni vyema mkapanda maua
mazuri na miti na ni lazima watu wa Mazingira wahakikishe kuwa wakati wote kuna
mtu muhimu wa kusimamia mazingira. Pongezi kubwa kwa mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi
na mkandarasi ni vyema kuwatumia makandarasi wazawa kama hawa. Nimefarijika
sana, Soko hili ni la Mfano wengine waje
kujifunza katika kulinda
mazingira".amesema Mhe Jafo
Akitoa shukrani Mkuu wa MKoa wa Dodoma Mhe. Anthony
Mtaka amemshukuru Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na
Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo (Mb kwa kutembelea na kujionea jinsi ujenzi
wa Machinga Complex unavyoendelea.Aidha Mhe. Mtaka amemwahidi Mhe.Waziri
kuzingatia na kufanyia kazi maelekezo yake yote.
Mhe. Mtaka amemfahamisha Mhe. Waziri kuwa yeye na viongozi
wengine wamejitahidi kuhakikisha kuwa wafanya biashara katika Soko hilo ni
machinga kwani Watu watakaokuwa hapa ni
watu wa kawaida kabisaaa. “Tunataka machinga ambaye mvua jua na mvua vyote vya kwake. Benki ya NMB imeahidi kutoa
Tsh. 500,000/- kwa kila mfanya mmachinga atakayekuja hapa. Hivyo nitoe Wito
kwa Vijana wote wa machinga ambao ni zaidi ya machinga 6000 wote waje
kufanya biashara zao humu.Sitaki mtu abaki huko mtaani ” Amesisitiza Mhe. Mtaka.
Mwisho.
Comments
Post a Comment