Mradi wa Bwawa la maji Membe- Chamwino, Utakaogharimu Tsh. 11.965 Bln Kuanza hivi Karibuni
Akikabidhi mradi wa ujenzi wa bwawa la maji la Membe, mradi utakaogharimu kiasi cha Tsh. 11.965 bln, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya amesema, mara bwawa hili litakapokamilika litawezasha umwagiliaji wa hekari 8000.Bwawa litakuwa na maji kwa mwaka mzima. Mhe.Msuya, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo. Aidha Mhe. Msuya amemshukuru Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kwa kuridhia fedha hizi zije kwenye mradi wa bwawa la maji la Membe. Mradi huu ulisanifiwa mwaka 2016 lakini kwa kipindi chote chote hicho haukutekelezeka hadi mwaka huu ambapo utaanza 01/9/2022 na kukamilika 01/9/2023.Miradi huu ukikamilika Wilaya ya Chamwino tutakuwa na chakula cha kutosha. Kutakuwa na utaratibu maalum wa kuingia kwenye bwana nalo bwawa hili litatengeneza ajira kwa vijana.Ombi langu kwa Wanamembe ni kutoa ushirikiano katika mradi huu kwani ni wenu. Ombi...