MIRADI 6 HALMASHAURI YA WILAYA BAHI YAPITISHWA NA MWENGE WA UHURU 2022

Ikiwa ni siku ya kwanza tangu Mwenge wa Uhuru uingie na kuangaza Mkoani Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imekuwa Halmasuri ya kwanza  kuangaziwa na Mwenge wa uhuru.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha viongozi wa mwenge wa uhuru mwaka 2022 , Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa Wilaya ya Bahi ina miradi sita ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru.

Mhe.Munkunda ameitaja miradi hiyo kuwa mradi wa uogeshaji wa Mifugo.Zaidi ya 60% za makusanyo ya Halmashauri ya Bahi hutokana na Mifugo.

Mradi wa Shule shikizi Mpamantwa, mradi huu umesaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kutembea mbali mkubwa kwenye shule mama. Aidha mradi huu umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la awali na darasa la kwanza.

Mradi wa tatu ni wa kikundi cha Vijana Technician Corporation, mradi huu ni wa vijana ambao awali walikuwa mafundi umeme ila baadae wakaamua kaunzisha duka la vifaa vya umeme, mradi huu umewanufaisha vijana kwani umeongeza ajira.

Mradi wa nne ni mradi wa maji  ambao lengo lake ni kuboresha huduma za usambazaji maji katika mji wa Bahi na hatimaye kuongeza uzalishaji wa maji toka lita 377,000 hadi lita 905,000/.

Mradi wa tano ni mradi wa utoaji huduma za mionzi (X-ray na Ultrasound ) hospitali ya wilaya.kabla ya kuanzishwa mradi huu wagonjwa wengi walikuwa wanaenda kupata huduma hospitali ya mkoa (general Hospital Dodoma).Tangu huduma hii ianze 15/6/2022, jumla ya wagonjwa 413 wamenufaika na huduma ya mionzi ya X-ray na wagonjwa 242 kwa upande wa Ultrasound.

Mradi wa Sita ni Ujenzi wa Boksi Kalavati la Mzizima  lenye urefu wa mita 35.15 n1 upana mita7.7,kimo mita 4.0 upana wa mita 4.0. Ujenzi wa kalavati /kivuko hiki utasaidia barabara ya Chigongwe - Chipanga kupitika wakati wote na kuondoa tatizo la kusimama kwa shughuli za usafiri na usafgirishaji wakati wa mvua na watu kusombwa na  maji ya mto.

Miradi yote hiyo sita ilipitiwa na viongozi wa Mwenge wa Uhuru na Kupitishwa japo baadhi ya miradi ilihitaji marekebisho. Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Bahi na kuwakumbusha kusensabika mara ifikapo 23.8.2022.

Mwisho































Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA