Akikabidhi mradi wa ujenzi wa bwawa la maji la Membe, mradi utakaogharimu kiasi cha Tsh. 11.965 bln, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya amesema, mara bwawa hili litakapokamilika litawezasha umwagiliaji wa hekari 8000.Bwawa litakuwa na maji kwa mwaka mzima.
Mhe.Msuya, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo. Aidha Mhe. Msuya amemshukuru Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kwa kuridhia fedha hizi zije kwenye mradi wa bwawa la maji la Membe. Mradi huu ulisanifiwa mwaka 2016 lakini kwa kipindi chote chote hicho haukutekelezeka hadi mwaka huu ambapo utaanza 01/9/2022 na kukamilika 01/9/2023.Miradi huu ukikamilika Wilaya ya Chamwino tutakuwa na chakula cha kutosha.
Kutakuwa na utaratibu maalum wa kuingia kwenye bwana nalo bwawa hili litatengeneza ajira kwa vijana.Ombi langu kwa Wanamembe ni kutoa ushirikiano katika mradi huu kwani ni wenu. Ombi kwa Mkandarasi kutekeleza mkataba kwa wakati na kwa viwango na makabaliano ya mkataba.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Aziza Mumba ( Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji) amesema ni furaha sana kuupokea mradi huu , tumepewa upendeleo wa hali ya juu maana kuna halmashauri nyingi nchini lakini Mkoa wa Dodoma umepata fursa hii adhimu.
Bwawa la maji la Membe litakuwa mkombozi kwa uchumi wa wananchi wa Dodoma, na litapunguza changamoto za ajira kwa vijana kwani watazalisha chakula mara 3/4 kwa mwaka. Mkoa utakuwa karibu sana kwenye usimamizi.Wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kuna kazi za elimu na za mikono hii hela ibaki hapa Membe na Mkoani Dodoma,wananchi wawe tayari kufanya kazi hizo.
Akielezea mradi huo Meneja wa Mradi Eng.Raphael Laizer, ameeleza kuwa watachimba tuta lenye kina cha 451 m, Upana 12 na kimo cha 110-117m hii ni kulingana na hali halisi ya mwinuko wa ardhi. Mradi huu utakamilika ndani ya miezi 12. Kutakuwa na sehemu ya mifugo na matoleo ya maji ya kunywa ya watu.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Tume ya umwagiliaji Mhandisi mkazi Eng. Salehe Ramadhani ameeleza kuwa Bwawa la Membe litakuwa na ukubwa. wa 5.1mln cubic meters na litagharimu Tsh.11.965 bln.
“Kulingana na maagizo ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe mradi
huu utakuwa shirikishi.Kutakuwa na vikao vya tathimini. Kulikuwa na Kandarasi 30 zilizo omba kazi hii ila kandarasi Nakuroi Contractors ndio waliopata fursa hii na mhandisi Daniel Marishi ndie atakayekuwa msimamizi wa kandarasi hii”.Amesisitiza Eng.Salehe.
Nae Project coordinator Eng. Dani Marishi ameomba ushirikiano toka kwa Serikali ya Mkoa pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Membe, kilichopo kata ya Membe Halmshauri ya Chamwino.
Comments
Post a Comment