Mwenge Wa Uhuru Wamulika Dodoma,Kukimbizwa Km 1162
Mwenge wa Uhuru leo umeingia Mkoa wa Dodoma , Makao Makuu ya Nchi ambapo utakuwa Mkoani hapo kwa kipindi cha Siku nane kuanzia tarehe 16/8 hadi 23/8/2022.
Akizungumza baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema mwaka huu 2022 , Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dodoma utapita katika Wilaya saba na halmshauri nane za mkoa wa Dodoma ambazo ni Bahi, Dodoma Jiji, Chemba, Kondoa (V), Kondoa Mji, Chamwino, Mpwapwa na kumalizia Kongwa.
Ukiwa Mkoani Dodoma Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilometa 1162 na utapitia jumla ya miradi 39 ambapo kati ya miradi hiyo 39, 19 itawekewa mawe ya msingi, 10 itazinduliwa na 10 itatembelewa.
Akileleza thamani ya miradi hiyo Mhe. Senyamule amesema kuwa miradi hiyo ina thamani ya Tsh.14,156,615,332/-. "Miradi hii imetekelezwa kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Serikali Kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau wa Maendeleo".Amesema RC Senyamule.
Mhe. Senyamule amemshukuru, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia mkoa wa Dodoma fedha za miradi mingi ya kimkakati na mikubwa kwenye sekta ya miundo mbinu, Ujenzi, Usafirishaji, Kilimo, Elimu, Afya,biashara na huduma mbalimbali.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewapongeza na kuwakaribisha wakimbiza mwenge kitaifa Mkoani Dodoma na kuahidi kuwapa ushirikiano wote wataohitaji ili kufanikisha kazi yao.
Akitikia ukaribisho huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma ameeleza kuwa mwaka huu Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unasema Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo:Shiriki Kuhesabiwa, Tuyafikie Malengo ya Taifa. Aidha Bw. Geraruma ametaja Jumbe mbalimbali za Mwenge zitakazo wakumbusha wanchi kuhusu kuzuia rushwa, lishe bora msingi wa uchumi imara, zingatia usawa tokomeza ukimwi na magongwa ya mlipuko pamoja na ziro malaria inaanza na mimi nachukua hatua kutokomeza na dawa za kulevya -( tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya , ili kuokoa maisha.
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Dodoma ukitokea Mkoani Singida ambako ulikimbizwa kuanzia tarehe 09/8-15/8/2022.
Mwisho
Comments
Post a Comment