TIMU YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA KUSHIRKIKI SHIMIWI 2022
Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Dodoma wamekwenda kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yanayotarajiwa kuanza Tarehe 01 Oktoba hadi tarehe 16 Oktoba 2022 huko Mkoani Tanga . Mashindano hayo yatafanyika katika viwanja tofauti tofauti nane ambavyo ni Viwanja vya Mkwakwani ,Shule ya Sekondari Popatlal, Galanos sekondari, Bandari,Shule ya Tanga, Polisi Chumbageni na Viwanja vya Gymkhana. Mashindano hayao yakishirikisha timu mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete,riadha, kuvuta Kamba na kukimbia. geni rasmi katika mashindano ya SHIMIWI anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Kassim Majaliwa. Mashindano hayo yatafunguliwa rasmi Oktoba 5. Kauli mbiu ya mashindano ya SHIMIWI 2022 ni ``Michezo hupunguza magonjwa yasiyo ambukiza na kuongeza tija mahala pa kazi``. Nahodha wa timu ya Mkoa Bw.Victor Makayula, amesema timu ya mpira wa miguu imejipanga...