DODOMA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAKUNYWA MAZIWA SHULENI
Mkuu wa mkoa Mhe.Rosemary
Senyamule ndiye ambaye ndiye amekua
mgeni rasmi wa shughuli hiyo. Akizungumza
Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Dodoma upo tayari kutekeleza mpango
huo kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata glasi ya maziwa shuleni.
“Dodoma tupo tayari kuwa kama
mfano kwa mikoa mingine katika utekelezaji wa zoezi hili na kuhakikisha kila
mwanafunzi anapata angalau glasi moja ya maziwa akiwa shuleni kila siku”. Amesema
Mhe. Senyamule.
Zaidi ya nchi 70 ikiwemo Tanzania
zinaadhimisha wiki ya Unywaji maziwa Duniani ambapo mpango wa kuhakikisha kila
mwanafunzi anapata maziwa shuleni ulianza kutekelezwa nchini mwaka 2017 na
mpaka sasa takribani shule 48 zimenufaika huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “Faulu
Mtihani kwa glasi moja ya maziwa kwa siku”
“Juhudi ziendelee ili kila
mtoto afikiwe na mpango huu, kwani maziwa yana faida nyingi mwilini kwa Watoto
hasa kiakili” Ameongeza.
Hata hivyo, mgeni rasmi
ameendelea kusema kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha sekta za
kilimo, uvuvi na ufugaji zinafanya shughuli zake kisasa zaidi kwani mpaka sasa mikopo
yenye thamani ya shilingi Milioni 275 imetolewa kwa wafugaji kwa lengo la
kuimarisha ufugaji nchini.
Pia Serikali imesamehe kodi ya
ongezeko la thamani kwa vifungashio vya maziwa hivyo Serikali inatarajia kuona
gharama za maziwa na bidhaa zinazotokana na maziwa zinashuka bei ili kila mmoja
aweze kutumia bidhaa hiyo kwa urahisi kwani mtu mmoja anahitaji kunywa angalau
lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini kwa takwimu zilizopo sasa, mtu mmoja
anakunywa lita 60 tu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
mifugo na uvuvi Dr. Charles Mhina amesema lengo la siku hii ni kuhamasisha
unywaji wa maziwa hasa kwa Watoto waliopo shuleni. Ameongeza kwa sasa lita za
maziwa zipatazo Bilioni 3.4 zinazalishwa nchini lakini bado watanzania hatunywi
maziwa.
“Tunapanga utaratibu wa
kuwawezesha wadau kupatikana kwa kiasi kikubwa cha maziwa kukidhi idadi ya
wanafunzi wote waliopo shuleni” Dr. Mhina
Siku ya unywaji maziwa shuleni
inatekelezwa kufuatia wito wa Shirika la Chakula na kilimo ulimwenguni (FAO) ambapo
kwa Tanzania, Bodi ya maziwa nchini (TADB) ambayo inaratibu mpango huu ikiwemo
kufanya kampeni mbalimbali za uhamasishaji unywaji maziwa shuleni ambapo wadau
mbalimbali wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kufadhili mpango huu kwa
kugawa maziwa kwa wanafunzi kila siku ambapo mpaka sasa paketi 299
zimeshagawiwa kwenye shule kadhaa huku lita 6500 zikipokelewa kutoka kwa wadau
hao.MWISHO
Comments
Post a Comment