TIMU YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA KUSHIRKIKI SHIMIWI 2022
Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Dodoma wamekwenda kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yanayotarajiwa kuanza Tarehe 01 Oktoba hadi tarehe 16 Oktoba 2022 huko Mkoani Tanga .
Mashindano hayo yatafanyika katika viwanja
tofauti tofauti nane ambavyo ni Viwanja vya Mkwakwani ,Shule ya Sekondari
Popatlal, Galanos sekondari, Bandari,Shule ya Tanga, Polisi Chumbageni na
Viwanja vya Gymkhana. Mashindano hayao yakishirikisha timu mbalimbali kama vile
mpira wa miguu, mpira wa pete,riadha, kuvuta Kamba na kukimbia.
Nahodha wa timu ya Mkoa Bw.Victor Makayula, amesema timu ya mpira wa miguu imejipanga kurudi na tshindi kutokana na kujiandaa vema kukabiliana na wapizani wao. ``Tumejipanga vyema kwani tulikua tunafanya mazoezi kila siku na vijana wangu wote wapo imara kabisa, Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule ategemee vijana wake tutarudi na Kombe kwani tunakwenda na kauli mbiu yetu ya Dodoma, Fahari ya watanzania, hivyo lazima tuiheshimishe Makao Makuu ya nchi.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa
wa Dodoma Dkt . Fatuma Mganga, Katibu Tawala msaidizi – Utawala Bw. Alois
Muogofi amewataka wanamichezo hao kujiamini na kuuwakilisha vyema Mkoa wa
Dodoma ambayo ndio makao makuu ya nchi.Aidha kwa niaba ya Dkt. Mganga, Bw.
Muogofi amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awatunze,awaongoze vyema ili
waweze kushinda.
Comments
Post a Comment