SOKO LA MACHINGA KUANZA RASMI OKTOBA 30
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya kikao na machinga wanaotarajiwa kufanya biashara katika soko la machinga lililopo barabara ya Bahi, lengo kuu likiwa kusikiliza na kutatua kero zao. Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa ameongozana na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri, Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na viongozi wanaosimamia soko hilo kutoka katika Halmashauri ya Dodoma Jiji. Mkuu wa Mkoa, ameanza kikao kwa kusikiliza kero kadhaa zinazowakabili machinga hao wakati wakisubiri kuhamia katika soko hilo. Miongoni mwa kero hizo ni pamoja na baadhi ya wafanya biashara kupangiwa vizimba ambavyo haviendani na biashara zao, baadhi ya machinga kukosa mikopo, machinga wa vitabu na magazeti kukosa vizimba, baba na mama lishe kukosa vizimba, daladala kushusa abiria eneo hilo, n.k Kero hizo zimepata majawabu kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Jiji Bw. Msangi pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu u...