WANANCHI WASISITIZWA KUJISAJILI PEMBEJEO ZA RUZUKU
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha kutathmini mwenendo wa zoezi la usajili wa wakulima kwenye mfumo kwa ajili ya kupata mbolea na pembejeo za kilimo kutoka Serikalini kwa bei punguzo(ruzuku) kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wakuu
wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Jiji la Dodoma pamoja na maafisa ugani.
Baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya hali ya kilimo kwa sasa kwa Mkoa wa Dodoma
pamoja na zoezi la usajili wa wakulima kwenye mfumo kwa ajili ya pembejeo za
kilimo za ruzuku, Mhe. Senyamule amesema;
“Twendeni tukahamasishe
wananchi wajisajili kupata na kutumia mbolea, muwape elimu ya namna ya kutumia
mbolea ya ruzuku kwani nguvu ya Serikali kwa sasa inakwenda kwenye kilimo”
Hata hivyo, amewataka maafisa
ugani kufanya oparesheni ya kujiwekea malengo kwamba kwa siku lazima wasajiliwe
wakulima hamsini ingawa ana imani inawezekana kusajili wengi zaidi ya hao.
Akiwasilisha ripoti ya Kilimo
Mkoa pamoja na zoezi la usajili kwenye mfumo kwa Halmashauri zote, Katibu
Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji
Mkoa Bi. Aziza Mumba amesema kuwa, kutokana na changamoto ya muda mrefu ya
upatikanaji wa pembejeo na mbolea bora, Serikali imeandaa mwongozo wa kusimamia
mbolea ya ruzuku.
“Lengo hasa la Serikali ni
kumpunguzia mkulima gharama za pembejeo za kilimo kwani bei ambayo Serikali
itamsaidia mkulima wakati akihitaji kupata pembejeo za kilimo ni zaidi ya
asilimia 50” .Amesisitiza Bi.Aziza Mumba.
Kuhusu ripoti ya waliokwisha jiandikisha
kwenye mfumo wa kununua mbolea na pembejeo za ruzuku,Bi. Aziza amesema mpaka
sasa kiwango bado hakiridhishi kwani ni chini ya asilimia 50 huku akisisitiza
kuwa hakuna mbolea itakayouzwa nje ya mfumo wa ruzuku kwa mwaka huu wa kilimo.
MWISHO
Comments
Post a Comment