WATOTO 695,508 KUPATA CHANJO YA POLIO MKOANI DODOMA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma chini ya Idara ya Afya, imefanya kikao cha kamati ya afya msingi ikiwa ni katika kuhamasisha awamu ya nne ya utoaji wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Polio kwa Watoto wenye umri kuanzia miaka 0 hadi miaka 5. Chanjo hiyo itaanza kutolewa tarehe 1 Desemba mpaka 4, 2022. Chanjo hii kama ilivyokua ikitolewa kwenye awamu zilizopita, inatarajiwa kutolewa nyumba kwa nyumba ili kuweza kufikia idadi kubwa ya Watoto wenye uhitaji wa huduma hiyo ambapo matarajio ni kuchanja Watoto 695,508. Akihamasisha wazazi kushiriki kikamilifu kuwatoa Watoto wao wapate chanjo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema; “Dodoma tumefanya vizuri katika awamu zilizopita na leo tunajadili namna nzuri ya kwenda kutekeleza awamu hii ya nne. Mhe.Rais ametimiza wajibu wake kwa kutoa fedha na sisi tutekeleze jukumu hili. Nasisitiza chanjo ni salama, wazazi andaeni Watoto wote. Ni imani yangu tutakwenda kutoa elimu tutakayoipata hapa kwa wazazi wenye Watot...