"Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita ni Wananchi" Rais Samia Suluhu Hassan
Mhe. Rais nikupongeze kwa kazi za kitaifa na kimataifa
unazozifanya kwa manufaa ya Watanzania" Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.
Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhala wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Chemba.
Akizungumza, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewaeleza
wananchi wa Chemba kuwa mwelekeo wa
Serikali ya awamu ya Sita ni wananchi ambapo msisitizo mkubwa ni kwenye elimu,
maji, umeme,afya pamoja na kilimo.
Akizungumza miradi ambayo imefanywa na Serikali ya awamu ya
sita katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Mhe. Rosemary Senyamule ametaja miradi mbalimbali ambayo Mhe. Rais
ameifanya katika Halmashauri hiyo. Miradi hiyo ni pamoja na Elimu ambayo
inahusisha ujenzi wavymba vya madarasa pamoja na mikopo ya vyuo vikuu, afya,
kilimo, barabara pamoja na umeme.
Mhe.Senyamule amesema kuhusu sekta ya elimu,Mhe. Rais ametoa
kiasi cha Tsh.9.7 bln, amejenga chuo cha VETA kwa gharama ya Tsh. 2.2 bln na hivyo kwa mara ya kwanza
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imepata chuo cha VETA. Aidha ujenzi wa vyumba
vya madarasa 46 unaendelea na madarasa
hayo yatakamilika kabla ya mwezi Januari 2023 ili kuhakikisha wanafunzi wa
kidato cha kwanza wanaingia madarasani. Aidha katika kuhakikisha kuwa wanafunzi
wote wa vyuo vikuu wanaendelea na masomo Mhe. Rais ametoa Tsh.24.5bln ikiwa
mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
"Kwa Upande wa Sekta ya afya Mhe Rais ametoa Tsh. 3.3
bln na bado kuna mradi wa kimkakati wa hospital ya Wilaya ambayo ujenzi wake
bado unaendelea kwa gharama ya Tsh.2.0 bln" RC Senyamule.
Mhe. Senyamule amesema kuwa Uchumi wa Wilaya ya Chemba unategemea sana Kilimo na
Ufugaji.Kwa kuwajali wananchi wa Chemba Mhe. Rais ametoa Tsh. 1.0 Bln kwa ajili
ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao ambalo ujenzi wake umekamilika.Hali
kadhakila Mhe.Rais kwa kuwajali wakulima ametoa mbegu na mbolea za ruzuku
pamoja,kwa kuwajali wafugaji Mhe. Eais ametoa fedha ambazo zimewezesha ujenzi wa Majosho ya kuogeshea
wanyama.
Aidha katika kukabiliana na kupanda kwa bei za vyakula Mhe.
Senyamule amemueleza Mhe. Rais kuwa kuanzia wiki ijayo wananchi wa Chemba
wameahidiwa kupata vyakula kwa bei rahisi.
"Kuhusu sekta ya maji, upatikanaji wa maji katika
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ni 32%, hata hivyo kuna miradi 11 ya maji
ambapo ikikamilika itapunguza changamoto hiyo, kwani itaongeza upatikanani wa
maji kufikia 55%. Pamoja na miradi hiyo 11 ujenzi wa bwawa la Farkwa ambalo
Serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan umetoa
jumla ya Tsh. 300 bln, mradi huu utatatua changamoto ya maji katika Halmashauri
za Bahi, Chemba, Chamwino, Kondoa pamoja na Jiji la Dodoma.
Akizungumzia barabara Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali ya
awamu ya sita imetoka kiasi cha Tsh. 3.3 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa
barabara za Halmashauri ya Chemba. Pamoja na hayo Serikali ya awamu ya sita
imetoa kiasi cha Tsh. 30 bln kuhakikisha kila nyumba katika Halmashauri ya
Chemba inapata umeme.
MWISHO.
Comments
Post a Comment