TUANZE KUTUMIA NISHATI MBADALA KUPUNGUZA UKATAJI MITI - MHE SENYAMULE Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa rai kwa wakazi wa Dodoma kuanza kutumia nishati mbadala ili kupunguza ukati wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa. Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kilichopo Ihumwa ikiwa ni mwanzo wa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti kwa Mkoa wa Dodoma. "Leo tupo hapa kutekeleza mpango wa Serikali juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni mwendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na wenzetu. Nitoe rai kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha tunasimamia maelekezo ya Serikali ya kuzuia ukataji miti bila vibali, tuanze kutumia nishati mbadala kama gesi kwa ajili ya kupikia kama anavyosisitiza rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan" Mhe. Senyamule alisisiza. Vilevile, Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Wakurugenzi ...
Posts
Showing posts from December, 2022
- Get link
- X
- Other Apps
WASIOPANDA MITI KWENYE MAENEO YAO KUCHUKULIWA HATUA Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa mazingira, leo tarehe 30 Desemba 2022, imetangaza kampeni maalumu ya upandaji miti katika Mkoa wa Dodoma lengo hasa likiwa ni kutimiza lengo la kampeni ya kuikijani Dodoma. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi uliopo kwenye jengo la Mkapa, ofisini kwake. “Sote tunafahamu kuwa msimu wa mvua umeanza hivyo, ni wakati sahihi kwa wananchi na wakazi wote wa Dodoma kutekeleza kwa vitendo Kampeni ya upandaji miti kuanzia ngazi ya Kaya, Kata, Vijiji, Vitongoji hadi ngazi ya Taasisi na msisitizo wa mwaka huu ni kwamba miti yote itakayopandwa hakikisheni inakua na kustawi vizuri” Amesisitiza Mhe. Senyamule Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amezitaja baadhi ya faida za uwepo wa miti ya kutosha katika mazingira yetu na Mkoa kwa ujumla kuwa ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na jami...
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 24 Desemba 2022 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya katika kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari, Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili. Amesema z awadi hizo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu. Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika maadili ya kumpendeza Mungu na wanadamu. “Lengo na dhumuni la Mhe. Rais ni kuona watoto wanasheherekea sikukuu kwa furaha na amani, kumbukeni kuwa chochote anachokifanya ni kwaajili ya watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ili watoto mpate elimu bora na kuongeza kiwango cha utafulu, hivyo mkiwa dar...
- Get link
- X
- Other Apps
DODOMA YAJIPANGA KUKABILIANA NA UTORO SHULENI 2023 Mkoa wa Dodoma umejidhatiti kukabiliana na utoro wa wanafunzi shuleni kupitia maazimio yaliyowekwa kwa mwaka 2023 kupitia kikao cha pili cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Rosemary Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Katika kikao hicho, agenda ya elimu imejadiliwa kwa kina na kupewa msukumo madhubuti ikiwa ni miongoni mwa ajenda nane za kikao hicho kilichojadili masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo bajeti ya Mkoa, Elimu, Afya, Kilimo, Maji na Mazingira. Mkoa wa Dodoma unakabiliwa na changamoto kubwa ya utoro kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari huku sababu kubwa zikitajwa kuwa ni ukosefu wa chakula shuleni, Wazazi/Walezi kutoipa thamani stahiki elimu hivyo kutowajibika kwa malezi ya watoto wao, Viongozi wa Vijiji kushindwa kutimiza wajibu wao wa kudhibiti utoro shuleni na umbali mrefu wa kwenda na kurudi. Akizun...