Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 24 Desemba
2022 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya katika kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba
ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari, Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili. Amesema zawadi hizo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu.
Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika maadili ya kumpendeza Mungu na wanadamu.
“Lengo na dhumuni la Mhe. Rais ni kuona watoto wanasheherekea sikukuu kwa furaha na amani, kumbukeni kuwa chochote anachokifanya ni kwaajili ya watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ili watoto mpate elimu bora na kuongeza kiwango cha utafulu, hivyo mkiwa darasani msikilize mwalimu na mkirudi kituoni muda wa jioni jisomeeni” Alisisitiza Mhe. Senyamule.
“Chochote unachokifanya fanya kwa bidii kila
mtoto ana ndoto na malengo yake ya baadae, Serikali inatambua mchango wenu ndio
maana Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa zawadi hizi za vyakula na kiasi cha fedha ili wote mfurahie sikukuu
ya Krismasi na Mwaka Mpya. Mhe. Senyamule aliongezea.
“Jukumu lenu ni pamoja na kuhakikisha watoto hawa wasoma ili kuyatumia madarasa yanayojengwa na Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili tuwe na kizazi chenye maadili mema ya kitanzania na ndoto za kutimiza malengo ya watoto wetu” Alifafanua Mhe. Senyamule.
Aidha mlezi wa kituo cha Safina Bi. Neckson William ameishukuru Serikali kwa kutoa zawadi za sikukuu kwa watoto.
“Tunaishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia kituo cha Safina tumefurahi sana kwakuwa tuna watoto ambao pia wapo nje ya Safina. Kituo kinawatoto kuanzia miaka miwili na mwaka huu tumefanikwa kupeleka Chuo Kikuu watoto wawili” Alisisitiza Bi. William
Kituo cha Safina kilianzishwa mwaka 2004 na
kina jumla ya watoto 40, wavulana 35 na wasichana 5 pia kitua hicho
kinawasaidia watoto ambao wanatoka katika mazingira magumu.
Comments
Post a Comment