MRADI WA KOFFIH WAIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

Idara ya Afya chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imefanya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ambaye amewakilishwa na Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Gugu katika Hoteli ya Vizano Jijini Dodoma. Mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri mbili za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Kongwa na Mpwapwa chini ya udhamini wa Taasisi ya nchini Korea inayojulikana kama KOREA FOUNDATION FOR INTERNATIONAL HEALTH CARE (KOFIH) ambapo wadau mbalimbali wa afya kutoka katika Halmashauri hizo wamehudhuria kikao hicho. Akifungua kikao hicho Bw. Gugu amesema tafiti zilizofanywa na Tanzania Demographic Health Survey ya mwaka 2022, inaonyesha viashiria vya huduma ya afya ya uzazi kwa Dodoma inafanya vizuri. Pia ameainisha idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya afya kwa Mkoa wa Dodoma ambavyo vimekua chachu ya utoaji wa huduma Bora za afya. "Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Dodom...