MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 16










Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Ally Senga Gugu  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba.

Makabidhiano hayo ya Mwenge wa Uhuru 2023 yamefanyika leo tarehe 29 Septemba 2023 katika Viwanja vya Bahi - Sokoni Wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

Akipokea mwenge huo Bw. Gugu amesema kuwa lengo kubwa la kuupokea mwenge ni kufanya uchechemuzi wa miradi pamoja kuhamasisha upendo, amani na ushirikiano.

Katibu Tawala huyo akizungumza muda mfupi baada ya kupokea mwenge huo wa Uhuru amesema kuwa utapita katika Wilaya zote saba (7) na Halmashauri  nane (8) zikiwemo Bahi, Chemba, Kondoa Dc, Kondoa Mji, Dodoma jiji, Chamwino, Mpwapwa na kumaliza ratiba kwenye Wilaya ya Kongwa.

Amesema mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa kwa kilometa elfu moja Mia nane na tini na tatu (1893) na katika mbio zake utapitia jumla ya Miradi arobaini na tano (45) ambapo miradi kumi na tano (15) itawekewa  mawe ya msingi na miradi kumi na tisa (19) inatarajiwa kuzinduliwa na kumi na moja (11) itatembelewa yenye jumla ya thamani zaidi ya Billioni 16. ikiwepo miradi ya sekta ya elimu,afya miradi ya utunzaji wa Mazingira.

Aidha, Bw. Gugu amesema  kuwa miradi hiyo ambayo itazinduliwa na mbio za Mwenge wa uhuru italenga kuwasaidia watanzania hususan wakazi wa maeneo husika.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga akitoa taarifa za mwenge katika Mkoa wa Singida kabla ya makabidhiano amesema umefanikiwa kuzindua miradi mbalimbali na mingine kuwekwa mawe ya msingi. 

Amebainisha miradi ambayo imetekelezwa katika Mkoa wa Singida na Wilaya zake ni pamoja na sekta ya Elimu, Afya, Utawala, Kilimo, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Barabara, Nishati na Maji.

Akizungumzia miradi amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Septemba  2023 miradi yenye thamani ya fedha kiasi shillingi Bilioni 224 imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Dkt.Mganga amesema sekta ya Elimu amesema kuwa Jumla ya sh.Bilioni 34.08 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu hususani ujenzi wa shule mpya za BOOST na shule mpya za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP pamoja na utoaji wa elimu bila malipo kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Nae, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa  Bw.Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa lengo la kukagua miradi hiyo ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha.

Amesema serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hasani,imekuwa ikipambana kutafuta fedha kwa kwa ajili ya maendeleo hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanasimamia miradi kwa thamani ya fedha inayotakiwa.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA