Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule mwishoni mwa wiki amefunga kongamano la kidini la waumuni wa Kiislamu (IJITIMAI) lililofanyika kwa takribani siku tatu katika Msikiti wa Gadaffi Jijini Dodoma.

Akifunga kongamano hilo Senyamule amewasisitiza wanawake waumini wa dini hiyo kuendelea kuliombea Taifa ili maadili yaendelee kuimarika kutokana na kumomonyoka na kuibuka kwa maadili yasiyo ya Kitanzania ambayo yanaharibu Utamaduni wa Nchi.

"Sisi ni wanawake tuna kazi ya kulea, kutunza, kufundisha tabia na kujenga watoto wetu, kwahiyo kazi hii tusiifanyie mzaha ni kazi ambayo ina nafasi nzuri kwa mwenyezi Mungu lakini maadili yanajengwa kama mtu ameiva ki-imani kwahiyo tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu watoto na vijana wetu wakuwe katika misingi na imani thabiti kwakuwa mtu mwenye imani anakuwa muadilifu. 

"Hata Serikali tunawadhamini watu walioshika dini kwasababu fedha za Serikali zitatumika vizuri na Miradi inatunzwa ili kila mtanzania ataendelea kufurahia na kufaidika na matunda ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa hata yeye ni mtu wa Imani na Upendo kwahiyo tuendelee kumuombea, kumtia moyo lakini zaidi tumsaidie kwa kujenga watu wenye maadili wataomsaidia kazi wasimsumbue kwa kufanya udokozi,"Mhe.Senyamule amesisitiza.

Kongamano hilo la IJITIMAI lililofanyika kwa siku tatu limewajumuisha wanawake wa kiislamu kutoka nchi za Afrika Mashariki ambapo Kongamano Hilo lilianzishwa rasmi mnamo Mwaka 1973 na hufanyika katika mikoa mbalimbali ndani ya Tanzania, pia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Mombasa nchini Kenya.

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA