Posts

Showing posts from July, 2024

NBC DODOMA MARATHON 2024 KUSAIDIA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amefanya Mkutano na waadishi wa habari kwenye ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma kuutangazia umma kuhusu mbio za NBC Marathon zinazotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 28 Julai 2024. Katika Mkutano huo, Mhe. Senyamule amebainisha lengo la mbio hizo ambazo zinatarajia kushirikisha takribani watu elfu kumi na mbili watakaoingia katika Mkoa wa Dodoma. “Lengo kuu la mbio hizi ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini pamoja na ufadhili wa masomo kwa wakunga kwa kupitia taasisi ya Bebjamini Mkapa. Saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza kwa kuchangia vifo zaidi vya wanawake.” Rc Senyamule Aidha, amesema kuwa mbio hizo zitaleta fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kwani idadi hiyo ya watu itahitaji malazi, chakula, mavazi, vinywaji na usafiri hivyo, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo. “Nichukue fursa hii kuwashawishi wananchi wa Dodoma kucha...

VYOMBO VYA USALAMA VYAAGIZWA KUCHUKUA HATUA VITENDO VYA KIKATILI KWA WATOTO

Image
Agizo limetolewa kwa vyombo vya usalama Mkoa wa Dodoma kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo vya kikatili vilivyoibuka hivi karibuni kwa watoto ikiwemo mauaji na kukatwa baadhi ya viungo vya mwili katika maeneo mbalimbali ya nchi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya na wananchi wa Kata ya Ipagala kwenye ofisi za Kata hiyo Jijini Dodoma Julai 22, 2024 wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili. “Jambo la Mtoto kutekwa halivumiliki na Serikali. Matukio haya yanafahamika na yanafanyiwa kazi na yeyote atakayebainika kuhusika, atachukuliwa hatua za kisheria. Natoa agizo kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka kwa matukio yanayosababisha vifo ili jambo hili lifike mwisho” RC Senyamule. Aidha, agizo hilo limefuatia kero iliyowasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa huyo na moja kati ya wakazi wa eneo hilo aliyelalamikia uwepo wa matukio hayo kwenye eneo lao sambamba na kuiomba Ser...
Image
  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya, leo Julai 12, 2024, amefanya kikao na Watumishi wa Ofisi yake chenye lengo la utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais kupitia Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa la kuanzisha klabu kwa ajili ya mazoezi ya viungo kwa Watumishi. Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma, kimeazimia kutekeleza maagizo hayo ambapo tayari jina la klabu hiyo limeundwa na itajulikana kama Dodoma RS Jogging Club na Mazoezi yanatarajiwa kuanza Julai 19, 2024. #dodomafahariyawatanzania #keroyakowajibuwangu

WARATIBU WA M-MAMA WANOLEWA DODOMA

Image
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya  Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI ) wametoa mafunzo  ya kuwajengea uwezo  maafisa habari ,waratibu na waelimishaji jamii ngazi ya Halmashauri na Mkoa wa Dodoma kuhusu  Mfumo wa m - mama . Mafunzo hayo yamefanyika Julai 10,2024 katika  ukumbi wa Mikutano uliopo   Nashera Hoteli na kufunguliwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Nelson Bukuru.  Akitoa mafunzo hayo Mwezeshaji  wa Kitaifa wa m-mama Bi. Kambarage Makuri amesema lengo la mafunzo hayo  ni kuongeza uelewa kuhusu mfumo wa m-mama, kuwawezesha washiriki kuwa na ujuzi na uwezo wa kuhamasisha jamii katika Mfumo huo kwa ufanisi pamoja na kutengeneza mpango kazi wa utekelezaji.  Kupitia mafunzo hayo wataalam hao wameweza kutengeneza Mpango Kazi wa Mkoa unaolenga kuwafundisha na kuwaelimisha viongozi wa ngazi zote pamoja na wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja  juu ya matumizi sahihi ya namba 115. &...