WARATIBU WA M-MAMA WANOLEWA DODOMA
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI ) wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa habari ,waratibu na waelimishaji jamii ngazi ya Halmashauri na Mkoa wa Dodoma kuhusu Mfumo wa m - mama .
Mafunzo hayo yamefanyika Julai 10,2024 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Nashera Hoteli na kufunguliwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Nelson Bukuru.
Akitoa mafunzo hayo Mwezeshaji wa Kitaifa wa m-mama Bi. Kambarage Makuri amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kuhusu mfumo wa m-mama, kuwawezesha washiriki kuwa na ujuzi na uwezo wa kuhamasisha jamii katika Mfumo huo kwa ufanisi pamoja na kutengeneza mpango kazi wa utekelezaji.
Kupitia mafunzo hayo wataalam hao wameweza kutengeneza Mpango Kazi wa Mkoa unaolenga kuwafundisha na kuwaelimisha viongozi wa ngazi zote pamoja na wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya matumizi sahihi ya namba 115.
&&&
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
Comments
Post a Comment