Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya, leo Julai 12, 2024, amefanya kikao na Watumishi wa Ofisi yake chenye lengo la utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais kupitia Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa la kuanzisha klabu kwa ajili ya mazoezi ya viungo kwa Watumishi.


Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma, kimeazimia kutekeleza maagizo hayo ambapo tayari jina la klabu hiyo limeundwa na itajulikana kama Dodoma RS Jogging Club na Mazoezi yanatarajiwa kuanza Julai 19, 2024.

#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA