TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA
Na Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs
Mwenyekiti wa Kanda ya Kati wa Chama cha Menejimenti ya kumbukumbu na Nyaraka Tanzania 'Tanzania Records and Archives Management Proffesionals Association (TRAMPA) Bw.John Kidasi amefanya kikao kazi na Viongozi pamoja na Wawakilishi (CRs) wa Menejimenti ya kumbukumbu na Nyaraka kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo tarehe 15 Desemba 2024.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jengo la Mkapa, lengo likiwa kukitambulisha chama hicho kwa baadhi ya wajumbe,wakifahamu vizuri wapi kilipotoka na muelekeo wake kwa siku zijazo.
#dodomafahariyawatanzania
Comments
Post a Comment