WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa maagizo kwa walimu (hawapo pichani) kuhusu kufundisha uzalendo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kusila Wilaya ya Bahi wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya miundombinu inayoendelea kutekelezwa katika shule hiyo mnamo Januari 28, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Kusila Wilaya ya Bahi wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya miundombinu inayoendelea kutekelezwa katika shule hiyo mnamo Januari 28, 2025.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma pamojna na Wataalamu mbalimbali waliombatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakifuatilia maagizo yaliyotolewa juu ya kufundishwa uzalendo wanafunzi wa shule ya Msingi Kusila Wilaya ya Bahi.
Picha juu na chini, baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwitikira katika Wilaya ya Bahi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) alipotembelea shuleni hapo kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu na kuzungumza nao juu ya somo la Uzalendo.
Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs.
Miongoni mwa sifa ya mzalendo ni Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu, majirani na marafiki kuipenda nchi yao na kujitoa kwa ajili yake pamoja na kuwafundisha watoto tamaduni za nchi husika.
Somo la uzalendo linapaswa kufundishwa Kwa Rika zote ikiwemo wanafunzi mashuleni, ndio maana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaagiza Walimu wa shule za Mkoani hapa Kuwafundisha wanafunzi uzalendo pindi tu wanapojiunga na shule Kwa ngazi ya awali na kuendelea.
Maagizo hayo ameyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Bahi katika shule ya Msingi Kusila na shule ya Sekondari Mwitikira alipotembelea kujionea utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika shule hizo.
Mhe. Senyamule Amesema " Suala la uzalendo lazima lihimizwe shuleni, ndio maana tuliagiza nyimbo za Taifa ziimbwe Kila siku, Sina hakika kama mnatekeleza kama tulivyokubaliana. Hawa watoto pamoja na kufaulu kwao lakini tunataka viongozi waaminifu na wanaoipenda nchi yao ya Tanzania.
"Kwa vyovyote vile, hayo yote yanafundishwa shuleni kwa hiyo, Walimu jitahidini kuwakazia sana juu ya uzalendo, anzieni Kuwafundisha tangu wakiwa madarasa ya chini kabisa na sio la 6 & 7 Ili wayashike katika umri ambao wataalam wanapendekeza kuwa mtoto anakuwa na uelewa wa kushika vitu Kwa haraka kati ya miaka 4-7 na sio rahisi kwao kusahau Kwa haraka", Amesema Senyamule
Katika hatua nyingine RC Senyamule ameuomba uongozi wa Kijiji Cha Kusila, kuandaa Mpango mzuri utakaowawezesha kujenga angalau maboma mawili na wakifika katika hatua ya umaliziaji Serikali ya Wilaya itakamilisha majengo hayo Kwa hatua za mwisho Ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa unaoikabili shule hiyo.
Hata hivyo umefanyika mkutano wa hadhara katika kata ya Mwitikira ambapo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Victor Swela ametumia Fursa hiyo kuwaasa wananchi kuachana na vitendo vya rushwa na kutoa taarifa pindi wanapobaini viashiria vya adui huyo wa haki Ili waweze Lusitania kazi Kwa wakati.
Kutokana na kijiji Cha Mwitikira kuwa pembezoni mwa Wilaya hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Peter Madialo ameuomba uongozi wa Mkoa kuwajengea kituo Cha polisi kijijini hapo Ili kuimarisha Hali ya Usalama ambapo Mkuu wa Mkoa ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji Ili kukamilisha kituo hicho na kuahidi kuwa pindi watakapoanza ujenzi huo ndipo atawakabidhi saruji hiyo.
Comments
Post a Comment