‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA

 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumzia matamanio ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa na usawa kwa makundi yote katika jamii alipokua akifungua mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kwa ajili ya kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, yatakayotolewa kwa kundi hilo na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) tawi la Jijini  Dodoma.






Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Mzee Kasore, akizungumzia namna Chuo chake kinavyofanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha wanawake wanaodahiliwa katika vyuo vya ufundi stadi wanaongezeka hadi kufikia 45% wakati wa hafla ya kufungua mafunzo ya muda mfupi kwa kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma.








Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Bw. Ramadhan Mattaka akizungumza na Wageni waliojitokeza kwenye hafla ya kufungua mafunzo ya muda mfupi kwa kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma juu ya kutoa hamasa kwa watu kujiunga na vyuo hivyo vilivyojengwa karibu kila Wilaya nchini.







Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma Bi. Fatma Madidi akitoa shukrani kwa VETA kwa niaba ya kundi hilo kwa kukubali kutoa mafunzo bure kwao yatakayokwenda kutoa Wataalamu watakaoisaidia jamii wakati wa hafla ya kufungua mafunzo ya muda mfupi yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma







Baadhi ya WAkuu wa Wilaya za Dodoma kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Dkt. Sophia Kizigo na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka walipomsindikiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwenye hafla ya kufungua mafunzo ya muda mfupi kwa kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma.






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Rosemary Senyamule akizindua rasmi mafunzo ya muda mfupi kwa kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma kwa kuoneshwa namna ya utengenezaji wa mapishi mbalimbali ya kuoka ikiwa ni moja ya kozi itakayotolewa kwa kundi hilo.










Pichani ni kundi la Wanawake na Samia ambalo litapatiwa mafunzo mbalimbaali ya muda mfupi kutoka Chuo cha VETA Jijini Dodoma wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.







Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na viongozi wengine kwenye meza kuu katika picha ya pamoja na wakufunzi wa kozi fupi zitakazotolewa kwa kundi la Wanawake na Samia mara baada ya kukamilika kwa hafla ya kufungua mafunzo hayo yatakayotolewa na VETA Tawi la Jijini Dodoma.








Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Mkoa wa Dodoma, kinatarajia kutoa mafunzo kwa kundi la ‘Wanawake na Samia’ wapatao 3000 linalounga mkono matamanio ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta Usawa wa kijamii na kijinsia ambayo ni kufikia mwaka 2030, ifike 50 kwa 50 kwa kila kundi kupata haki sawa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akifungua mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kwa ajili ya kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, zitakazotolewa kwa kundi hilo na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) tawi la Jijini  Dodoma.

“Mhe. Dkt Samia amekua akitamani kila kundi la Mtanzania lipate haki sawa ndio maana anasema hataachwa mtu nyuma awe ni mwanamke, mtu? mwenye ulemavu, mzee, kijana au mtoto. Anatamani Wanawake wa Tanzania washike uchumi sawa na wanaume, Makundi maalum ambayo yapo nyuma yashike uchumi sawa na makundi mengine”.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, amekipongeza Chuo cha VETA Dodoma kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo kwa sehemu yake yatahusu utalii, ujasiriamali na maadili kwa kundi hilo ambalo linatunza heshima ya jina la Mhe. Dkt Samia na lipo Makao Makuu ya Nchi ambayo inazidi kukua na kujengeka.

Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Mzee Kasore, amesema Chuo chake kinatoa mafunzo mbalimbali na eneo linalowekewa mkazo ni kuhakikisha wanawake wanaodahiliwa katika vyuo vya ufundi stadi wanaongezeka hadi kufikia 45% ambapo kwa sasa wapo asilimia 25 hadi 37 na wameanzisha programu za uwezeshaji wajasiriamali kwa akina mama ili kufikia lengo hilo.

Akizungumzia dhumuni la mafunzo hayo kwa kundi hilo, Mkuu wa VETA Dodoma Bw. Deodatus Orotha, amesema ni kuwapatia ujuzi wanawake wa Mkoa wa Dodoma ili waweze kutatua changamoto zao pamoja na familia lakini pia kuleta tija kwa Taifa. Amesema tayari wameshajisajili na mafunzo yataanza Machi 26, 2025 kwa muda wa wiki nne.

Nae, Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma Bi. Fatma Madidi amesema kuwa kundi lake linatoa shukrani kwa VETA kwa kukubali kutoa mafunzo hayo kwani kumsomesha mwanamke ni kuisomesha jamii na kupitia mafunzo hayo, watakwenda kutoa Wataalamu watakaosaidia Mkoa wa Dodoma, Tanzania na Dunia kwa ujumla.

Mafunzo hayo ambayo yatagharamiwa na VETA Dodoma, yanatarajiwa kuwanufaisha wanawake 3000 wa kundi hilo ambao watasoma kwa awamu ya wanawake 250 mpaka watakapokamilika ambapo wazo la kufanya mafunzo hayo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule



#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.