WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

 


Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akizungumza na Walimu wa shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma juu ya kutekeleza wajibu wao wakati wa kikao kazi cha ufuatiliaji wa maendeleo ya Taaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma Aprili 11, 2025.






Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwalimu Vicent Kayombo akielezea namna ufuatiliaji wa Elimu unavyofanyika katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao kazi cha ufuatiliaji wa maendeleo ya Taaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma Aprili 11, 2025.







Baadhi ya Maafisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha ufuatiliaji wa maendeleo ya Taaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma Aprili 11, 2025.








Pichani ni baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha ufuatiliaji wa maendeleo ya Taaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma Aprili 11, 2025.








Na. Hellen M. Minja,
       Habari – DODOMA RS

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amezungumza na Walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma juu ya kutekeleza wajibu wao kama ajira zao zinavyowataka kwa kuwafundisha Wanafunzi kulingana na kalenda ya Serikali.

Amezungumza hayo wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwalimu Vicent Kayombo chenye lengo la kuangazia taarifa mbalimbali za ufuatiliaji wa maendeleo ya taaluma kwenye shule zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo, kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma Aprili 11, 2025.

Kikao hicho ni mfululizo wa vikao kadhaa vya ufuatiliaji wa maendeleo ya Elimu katika Mkoa wa Dodoma ikiwa ni katika kufikia lengo la Mkakati wa Mkoa kuinua ufaulu katika Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi na Sekondari Mwaka 2025.



#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu










Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA