KAMATI YA USALAMA MKOA WA DODOMA YAFANYA ZIARA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO, KONDOA

 


Msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ukiingia kwenye Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya ziara ya siku mbili kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 9, 2026







Kikundi cha Ngoma ya asili kutoka Wilaya ya Kondoa kikitoa burudani wakati wa mapokezi ya Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ilipoingia kwenye moja ya Kambi za Pori la Akiba Mkungunero kwa ajili ya ziara ya siku mbili kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 9, 2026






Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Kambi ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya ziara ya siku mbili kuangalia maendeleoa ya shughuli za Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 9, 2026






Msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakifanya safari ya kitalii ndani ya Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika Wilaya ya Kondoa kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 9, 2026







Wanyamapori aina ya Pundamilia kama walivyoshuhudiwa na msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii ndani ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026





Wanyamapori aina ya Nyumbu kama walivyoshuhudiwa na msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii ndani ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026









Wanyamapori aina ya Tembo kama walivyoshuhudiwa na msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii ndani ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026






Mnyamapori aina ya Twiga kama alivyoshuhudiwa na msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii ndani ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026








Ndege aina tofauti wakiwa ndani ya Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa kama walivyoshuhudiwa msafara wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kitalii kuangazia shughuli za maendeleo ndani ya Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026







Kamati ya Usalama Mkao wa Dodoma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakipata mawasilisho kuhusu Pori la Akiba Mkungunero linalopatikana katika Wilaya ya Kondoa baada ya kufanya ziara ya siku mbili kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 9, 2026







Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea zawadi kutoka kwa Mwekezaji wa  Pori la Akiba Mkungunero linalopatikana katika Wilaya ya Kondoa baada ya kufanya ziara ya siku mbili kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026





Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu akiaga mara baada ya kutamatika kwa ziara ya Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kutembelelea wanyamapori la Akiba Mkungunero linalopatikana katika Wilaya ya Kondoa baada ya kufanya ziara ya siku mbili kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026







Kamati ya Usalama Mkao wa Dodoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara ya siku mbili kwenye Pori la Akiba Mkungunero linalopatikana katika Wilaya ya Kondoa kuangalia shughuli za maendeleo ya Utalii hususan Wanyamapori wanaopatikana katika Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Januari 10, 2026




Na Mwandishi wetu – DODOMA RS

Kamati ya Usalama Mkao wa Dodoma ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule sambamba na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Khatibu Kazungu, wamefanya ziara ya kuangalia maendeleo ya shughuli za Utalii hususan wanyamapori pamoja na miundombinu inayopatikana katika Hifadhi ya Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika Wilaya ya Kondoa.

Ziara hiyo ya siku mbili, ilianza Januari 09 hadi 10, 2026 kwa msafara ulioanzia kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Dodoma hadi eneo la Pori hilo linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inayojishughulisha na usimamizi na uhifadhi wa Wanyamapori, usimamizi wa mapori ya akiba na maeneo ya wazi ya wanyamapori, udhibiti wa majangili pamoja na kukuza utalii wa wanyamapori nje ya hifadhi za Taifa.

 Wakiwa katika moja ya kambi za Pori hilo, Kamati ya Usalama Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, walipokelewa kwa bashasha na kupata fursa ya kufanya utalii wa kuzunguka ndani ya Pori hilo lenye mtandao wa barabara zenye urefu wa zaidi ya Km 364 kuangalia wanyamapori wanaopatikana hapo ambao ni kivutio kikubwa cha Utalii wa ndani, nje ya Mkoa na hata nje ya nchi.

 Pori la akiba Mkungunero lilitangazwa rasmi mwaka 1996 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 743, linapatikana umbali wa Km 240 kutoka Jiji la Dodoma likiwa na aina kadha wa kadha za Wanyama pori kama vile Simba, Chui, Tembo, Nyati, Twiga, Pundamilia, Fisi, Swala, Tandala, Ngiri, Pofu, Nyumbu na wengine wengi huku likiwa na aina zaidi ya 249 za ndege.



#TakeDodomaToTheWorldAndBringTheWorldToDodoma
#DodomaFahariYaWatanzania
#AmaniYetuUstawiwetu
#WekezaDodomaStawishaDodoma
#KazinaUtuTunasongaMbele






























Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA