Posts

Showing posts from June, 2022

Watu Wenye Ulemavu Washirikishwe Kwenye Kila Hatua ya Zoezi la Sensa

Image
  Watu wenye Ulemavu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wakisikiliza Kongamano la Sensa na Watu wenye Ulemavu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa  Mwenyekiti wa Watu wenye Ulemavu Nchini Bw. Diwani Kimaya akizungumza wakati wa Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, akiwakaribisha Mkoani Dodoma wanakongamano  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Ndeliananga akizungumza wakati wa Kongamano hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye Ulemavu  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. George Simbachawene ( Mgeni Rasmi) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wakati wa Kongamano la Sensa na Watu wenye Ulemavu Washiriki mbalimbali wakisikiliza kongamano  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Tume ya Takwimu  imefanya Kongamano kubwa la   kuwajengea uwezo na kuwapa ujasiri watu wenye ulemavu...

Wajasiliamali Wapewa Mafunzo

Image
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma imetoa Mafunzo kwa wajasiriamali wadogo ambao wamewezeshwa mitaji ya biashara na Ofisi hiyo ambapo takribani wajasiriamali 20 walishiriki mafunzo hayo ambayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo walikuwa wataalamu kutoka  Shirika la  Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Dodoma.SIDO ina lengo la kuwasaidia wajasiriamali hao kufungua au kufanya biashara zenye tija. Akielezea namna ya kufanya biashara yenye tija, Bw. Stephano Ndunguru ambaye ni Mratibu wa mradi SIDO Dodoma, amewafundisha wajasiriamali uhusiano wa Biashara na familia kwani mfanyabiashara asipokua makini na uhusiano huo anaweza kuua biashara wakati lengo lake ni kukuza mtaji kila wakati. "Kuna tofauti kati ya mmiliki wa Biashara na Biashara yenyewe, hizi ni nafsi mbili tofauti zinazotakiwa kuheshimiana kwani unapokua na Biashara maana yake umejiari hivyo unapaswa kujilipa mshahara" Naye Msimamizi wa Fedha kutoka SIDO Dodoma Bw. Justine Kahemela...

ALAT WATEMBELEA JENGO LA MACHINGA

Image
Uongozi wa Kamati tendaji za Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT), hivi karibuni umetembelea Ujenzi unaoendelea wa jengo la Machinga   Complex, lililiopo eneo la Bahi Road Jijini Dodoma. Viongozi hao wapo Jijini Dodoma kwa   ajili ya kuhudhuria, vikao vya kiutendaji.Aidha pamoja na vikao hivyo viongozi hao, waliamua   kutembelea jengo la Machinga Complex ili kuliona na kujifunza. Wakiwa wameambatana na mwenyeji wao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, Mhe Mtaka aliwakaribisha kwenye mradi huo na kutoa shukrani na pongezi nyingi   sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia ujenzi huo na kuchangia   kiasi ctah Tsh.2.5 bil, ambazo zitatumika kumalizia ujenzi wa     mradi huo. Mhe. Mtaka alisisitiza kuwa mradi huu unatakiwa kujenga ujasiri kwa Halmashauri kubuni miradi mingi zaidi kwani watu wa kuiunga mkono wapo. Akielezea maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, ali...

Kata ya Ipagala Yawapongeza Walimu wa Shule Za Msingi Na Sekondari

Image
  Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali  pamoja na wanafunzi kutoka Kata ya Ipagala, leo wamepongezwa kwenye hafla iliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Bw. Gombo Kamuli Doto. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri- Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Omari Kipanga (Mb) ambapo mwenyeji wake alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Anthony Mtaka.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtemi Mazengo ambayo ni moja kati ya shule tano za Msingi za mfano nchini Tanzania. Akielezea Shule hiyo Bw. Gombo amesema kuwa Shule ya Msingi Mtemi Mazengo ni moja kati ya shule 5 za majaribio zilizojengwa na Serikali kwa lengo la kupima ufaulu kulinganisha na ule wa shule binafsi ambapo shule ina Madarasa 17, Miundo mbinu ya umeme na maji, maktaba, nyumba za walimu 4, ukumbi wa mkutano, viti na meza nzuri za kukalia waalimu pamoja na wanafunzi. Ujenzi wa shule hii umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1 ambao kati ya hizo Tsh.700 milioni zilitol...

“HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYESHINDWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA KUKOSA MICHANGO " RC -MTAKA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Anthony Mtaka, amekutana na Walimu Wakuu wa shule za sekondari zenye kidato cha Nne na Sita ili kuzungumza nao namna  bora  ya kujiandaa na Elimu bure kwa kidato cha Tano na Sita. Kikao hicho kilichohudhuriwa na takribani walimu wakuu 25 wa shule za sekondari za Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma ambazo zina   wanafunzi zaidi ya 3,000. Kikao kiliainisha michango inayotozwa na shule.michango ambayo huorodheshwa kwenye fomu ya kujiunga na Kidato cha Tano na ambayo kila mwanafunzi huhitajika   kuwa nayo pindi anapowasili shuleni kwa mara ya kwanza na kusababisha baadhi ya wazazi kushindwa kukidhi mahitaji hayo na kuacha kupeleka watoto wao shule. Walimu hao walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zitakazowakabili baada ya ondoleo la ada hizo kwani zilikua zikisaidia katika uendeshaji wa shule hasa kulipia ankara za umeme, maji na wasaidizi wa majukumu ya shuleni na kuongeza kuwa mahitaji ya muhimu kama vile Bima ya afya, kuagiza vite...