ALAT WATEMBELEA JENGO LA MACHINGA
Uongozi wa Kamati tendaji za Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT), hivi karibuni umetembelea Ujenzi unaoendelea wa jengo la Machinga Complex, lililiopo eneo la Bahi Road Jijini Dodoma. Viongozi hao wapo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria, vikao vya kiutendaji.Aidha pamoja na vikao hivyo viongozi hao, waliamua kutembelea jengo la Machinga Complex ili kuliona na kujifunza.
Wakiwa wameambatana na
mwenyeji wao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, Mhe Mtaka
aliwakaribisha kwenye mradi huo na kutoa shukrani na pongezi nyingi sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia ujenzi huo na kuchangia kiasi ctah Tsh.2.5 bil, ambazo zitatumika kumalizia
ujenzi wa mradi huo. Mhe. Mtaka alisisitiza kuwa mradi
huu unatakiwa kujenga ujasiri kwa Halmashauri kubuni miradi mingi zaidi kwani
watu wa kuiunga mkono wapo.
Akielezea maendeleo ya mradi
huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, alisema kwa sasa Ujenzi
upo kwenye awamu ya pili ya kukamilika na unatarajiwa kufanya kazi kwa saa 24
na mpaka kufikia Juni 30 mradi utakua umekamilika,ili ifikapo Julai Mosi, mradi
uwe umezinduliwa rasmi kwa wafanyabiasha kuanza kuutumia.
Akizungumzia mradi huo, Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa, mradi huo utasaidia
Halmashauri ya Dodoma kuongeza mapato, kwani kwa kipindi cha Mwaka mmoja, mradi unatarajiwa kuingiza kiasi cha
Milioni 100 ambazo zitakazotokana na
ushuru wa huduma mbalimbali zitakazokua zikitolewa mahali hapo. Mhe. Shekimweli
ametaka mradi huu kutumika kama Mfano wa
kuliweka Jiji katika mwonekano wa kuvutia na utumike kama sehemu ya utalii wa
ndani ya Mkoa.
Mwenyekiti wa ALAT Bw. Murshid Ngeze, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake kwa mradi huo na kuahidi kuwa watakuja kujifunza kupitia mradi huo. Aidha Bw. Ngeze ameitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa inasimamia vizuri mapato yatakayopatikana kutokana na mradi, kusimamia vizuri hali ya usalama kwenye eneo hilo kwa kuwa Biashara itafanyika kwa saa 24 pia ameshauri kuanzishwa mpango wa kutoa Mafunzo kwa wajasiriamali wanaotarajiwa kufanya biashara katika jengo hilo.
MWISHO
Comments
Post a Comment