IBADA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA MSAIDIZI RASILIMALI WATU MKOA WA DODOMA
















Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki kwenye mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala Msaidizi (Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu) Bw. Aloyce Mwogofi katika ibaada ya mazishi iliyofanyika Mkoani wa Njombe, Kijiji cha Itulike Kata ya Ramadhani.

Akizungumza na wafiwa na waombolezaji Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewataka waombolezaji kuiga mwenendo wake kwa kuiga mambo mema yoye aliyotekeza enzi za uhai wake.

“Mzee Mwogofi alikuwa ni mchapa kazi kwa asili yake, muadilifu na mfano wa kuigwa kuanzia vitendo, mavazi, nidhami na kwa kuwa kiongozi wa wa utumishi aliongoza wengine kwa mfano”Alisisitiza Bi. Senyamule.

Kama Serikali tunasema mapengo haya zibiki kwa maana hatutampata Mzee Mwogofi mwingine lakini tunaomba Mwenyezi Mungu atusaidie tupate mtu ambaye hatutaona hasara kubwa ya kumpoteza Mzee Mwogofi kwa maana ya alivokuwa.

"Mungu awashike Mkono familia awatie nguvu endeleeni kumtegemea Mungu leo tunamlaza Mzee wetu tuendelee kuiga mfano wa mzee wetu na tuige mema yake aliyokuwa anayanafanya” Alisisitiza Mhe. Senyamule .

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema tunaomtegemea Mungu tunaamini tunaeda kupata faraja kuu na tunaendelea na kazi  itoshe kusema kwamba mzee Mwogofi alikuwa ni mtu mwema akipenda upendo utamalaki katika eneo letu la kazi na hata nje ya kazi, hivyo tumempoteza mtaalamu katika utumishi.

Marehemu Aloyce Mwagofi alishawahi kufanya kazi katika Ofisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Sheria na Katiba, Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kama katibu Tawala Msaidizi seksheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasimali watu.







Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA