MHE. SENYAMULE AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LATRA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amezindua rasmi Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini
LATRA katika kikao cha kwanza cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa LATRA makao makuu
Dodoma.
Akizungumza na wafanyakazi Senyamule amesema anawapongeza kwa kukamilisha taratibu za kisheria za kuunda baraza hili na Kusajiliwa
na Kamishna wa kazi viongozi wa chama cha cummunication and workers traders
union (COWTU) Taifa na Tawi la LATRA kwa
kuwezesha kufikia makubaliano na Menejimenti ya LATRA kwa kusaini mkataba na
kuunda baraza la kwanza la wafanyakazi wa Mamlaka hii
‘’Katika kuendeleza mshikamano hapana budi Menejimenti
ihakikishe kwamba haki za msingi za mtumishi zinatolewa juhudi zitolewe katika kujifunza kujiendekeza
kimasomo ili kuendeleza ufanisi wa kazi na kujiwekea misingi imara ya kujenga
utumishi wa umma uliombora.
‘’Mfanyakazi ambaye ni mweledi na mwelewa anarahisisha kazi kwa kiongozi wake na kuifanya kuwa rahisi. Kila mmoja anatakiwa kuwa mfano wa kuingwa mahali pa kazi ili hata mtu anaweza kumsoma utendaji wake na kazi na ueledi wake wakati wa kazini
Naye Habibu Suluo Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakzi na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Amesema kuwa wana mkataba mpya ambao unajumisha wafanyakazi wa Mkoa yote 26 pia Mamlaka ilianzishwa na sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 2019 iliyoanza kutekeleza majukumu yake tarehe 29 April 2019.
Comments
Post a Comment