DODOMA KUWA KITOVU CHA BIASHARA NCHIN
Mkoa wa Dodoma umezindua Baraza la Biashara la Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule kuzungumzia mikakati ya kuuinua Mkoa kiuchumi.
Uzinduzi huo umeambatana na mawasilisho kutoka kwa wadau mbalimbali wa Biashara wakiwemo Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Baraza la wawekezaji na wadau wengine.
Wakati wa hotuba yake
ya ufunguzi wa mkutano huo, Mhe. Senyamule amesema;
"Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amepunguza sheria kandamizi kwa Wafanyabiashara, ameendelea kuleta wawekezaji kutoka nje na wanaingia kwa wingi nchini. Mkoa wa Dodoma tunataka tuwe na mchango Mkubwa kwenye Biashara hivyo ni matarajio yangu Baraza la Mkoa litakua bora na lenye utashi wa kipekee kwenye makao makuu ya nchi" Amesema Mhe Senyamule
Amewataka wajumbe wa Baraza hilo ngazi ya Wilaya kwenda kufanya vikao vya mabaraza pamoja na wale wa Halmashauri, Wakurugenzi wakafanye vivyo pia. Amewataka waende wakatenge maeneo ya uwekezaji ambayo yatavutia wageni watakapohitaji kwenda kuwekeza kwenye Halmashauri zao.
Aidha, Katibu Tawala
Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, ameainisha lengo kuu la Baraza pamoja na
malengo madogo madogo;
" Lengo kuu la Baraza hili ni kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha Biashara nchini huku malengo madogo yakiwa ni kuwa na mpango mkakati wa kufanya kazi ndani ya miaka mitatu, kutangaza shughuli za Biashara na fursa za uwekezaji kupitia vyombo vya biashara, kuongeza idadi ya uwekezaji unaofanyika Dodoma, maeneo ya uwekezaji yaliyotwaliwa yapimwe ili yaboreshwe, mabaraza ya Wilaya yaboreshwe pamoja na kuongeza wafanyabiashara" Ameainisha Dkt. Mganga
Akiwasilisha maazimio
ya Mkutano huu, Katibu Tawala Msaidizi sekta ya Biashara na Uchumi Mkoa Bi. Aziza
Mumba amesema;
" Maazimio ya Mkutano huu ni kuanzishwa kituo cha huduma ya pamoja cha wafanyabiashara, kuendeleza maeneo ya burudani, TNBC waendelee kujengwa uwezo mabaraza ili yawe imara na taarifa za kina za kila mfuko zipatikane na kusambazwa kwa wajumbe' Amesema Bi Mumba
Miongoni mwa faida za uwepo kwa Baraza la Biashara zilizoainishwa wakati wa wasilisho la TNBC lililofanywa na Meneja wake Bw. Willy G. Magehema ni pamoja na kukuza uwazi na utawala bora, kurahisisha utekelezaji wa maboresho ya kisera na kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi katika maandalizi ya Mipango ya biashara.
MWISHO
Comments
Post a Comment