JITIHADA NDO CHACHU YA MAFANIKIO "DKT MGANGA"
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amefungua
rasmi
mkutano wa kutoa mrejesho wa kazi zilizofanyika katika awamu
ya kwanza na ya
pili ya utafiti wa kutumia mbinu za vinasaba katika
ufuatiliaji wa malaria katika
kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Mkapa.
Akizungumza na Wajumbe walioshiriki kwenye kikao hicho, Dkt.
Mganga
amesema kazi ya uchakataji sampuli zilizokusanywa mwaka 2021
imekamilika
na matokeo zaidi yalitolewa kwenye mkutano wa wadau
uliofanyika mwezi mei
2022.
“Jitihada zenu mnazoendelea nazo ndizo zitakazokuwa chachu
ya kufanikisha
kazi muhimu kwa nchi yetu mchango mkubwa unatolewa na wadau
mbalimbali
katika mapambano dhidi ya malaria, katika ngazi ya Mkoa na
Halmashauri na
katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Napenda kuzishukuru taasisi na mashirika yote yanayohusika
na Utafiti na
Taasisi ya Bill and Melinda Gates kwa kutoa ufadhii kwa
ajili ya kutekeleza utafiti
huu, nawaomba muongeze juhudi ili tuweze kutokomeza malaria”
amesema Dkt
Mganga.
Hata hivyo Mtafiti Mkuu wa ukusanyaji taarifa Mkoa wa Dodoma
2022 Dkt.
Deusdedith Ishengoma amesema kuwa wanatekeleza Utafiti wa
kufuatilia
Ugonjwa wa Malaria Tanzania Bara kwa kutumia mbinu ya
vinasaba MSMT
(Molecular Surveillance of Malaria in Mainland Tanzania) na
lengo kuu la Utafiti
ni kuchunguza mabadiliko ya vimelea vya malaria ili kubaini
Kama mbinu
wanazotumia kupambana na Ugonjwa huo zinafanya kazi
ipasavyo.
“Utafiti huu unafanyika kwa lengo kufuatilia ubora na uwezo
wa dawa za kutibu
Ugonjwa wa Malaria pamoja na ufanisi wa vipimo vya malaria
vya papo kwa
papo (performance of rapid diagnostic tests for malaria”
Amesema
Dkt. Ishengoma
Ameongeza kuwa kazi ya kukusanya Sampuli na Takwimu
ilifanyika katika vituo
kumi vya kutolea huduma za kiafya kwa kila mkoa na kazi hii
ilitekelezwa na
wafanyakazi wa vituo hivyo chini ya Usimamizi wa Waganga
wakuu wa Mikoa na
Halmashauri wakisaidiwa na waratibu wa malaria wa Mikoa.
MWISHO
Comments
Post a Comment