MAFANIKIO YA SERIKALI AWAMU YA SITA KATIKA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA






 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule  amesema sekta ya afya imeendelea kuimarika na kupata mafanikio kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji  katika  maeneo ya utoaji huduma na ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya chini ya Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mkapa katika muendelezo wa Programu maalumu ya kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma Mhe. Senyamule amesema,

“kumekuwa na kituo cha Damu Salama Kanda ya kati kilichopo Mkoani Dodoma, uwepo wa kituo hiki umerahisisha upatikanaji wa damu salama na mazao ya damu na hivyo kusaidia katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya Watoto wachanga ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika kusafirisha sampuli za damu Kwenda Maabara Kuu ya Taifa iliyopo Dar- es Salaam.”  

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji  Dkt. Alphonce B. Chandika amesema katika kipindi cha miaka miwili cha Serikali awamu sita Hospitali ya Benjamin Mkapa imepiga hatua kubwa sana  imefanikisha kuimarisha kwa huduma ya upandikizaji wa Figo kwa idadi ya Wagonjwa 31  na kuendelea vizuri na afya zao.

“Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo na uwepo kwa Vifaa vya maradhi ya Moyo  pia Maabara Maalumu ya kuchunguza na kutibu maradhi ya Moyo imewezesha kubaini Ugonjwa kwenye Moyo hususani Mishipa midogo midogo inayopeleka damu kwenye Moyo na mara nyingi Wananchi huwa wanapata hayo maradhi na ni vigumu kugundua bila Maabara, Wagonjwa wenye matatizo ya Moyo 758 wameweza kuhudumiwa njia ya Maabara hii kati yao 12 wamepatiwa huduma ya Upandikizaji wa Betri kwenye Moyo kutokana na mapigo ya Moyo kuwa chini, Watoto waliozibwa matundu kwenye Moyo 10 na kusinyaa kwa Mshipa unao Lisha Moyo Damu (Stent) 52. Dodoma kwa  sasa iko imara katika kutoa Huduma ya matibabu ya Moyo” Amesema Dkt. Chandika

Dkt. Chandika  amesema Serikali awamu ya sita kwa kuweka Bajeti na usimamizi  imefanikisha Hospitali kuwepo kwa Huduma ya Vipandikizi kwenye Magoti na Nyonga  (Hip and total Knee Replacement) kwa Wagonjwa 53 walionufaika mpaka sasa.

Hata hivyo Hospitali ya Benjamin Mkapa inajivunia Mafanikio ya awamu ya sita kwa kuwezesha upatikanaji wa Huduma za  Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu kwa Wagonjwa 549 na Upasuaji Uti wa Mgongo kwa wagonjwa 415.

Aidha,Serikali inaendelea kutekeleza mrandi mingine katika  Hospitali ya Benjamini Mkapa  kwa kujenga Jengo la Mionzi Tiba unaogharimu Shillingi Billioni 28 na Serikali imetoa Shillingi 2.9 kwa malipo ya awali kwa Mkandalasi  na Ujenzi umefikia asilimia 15.6%. Amesitiza Dkt. Chandika.

MWISHO.




Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA