MAFANIKIO YA SERIKALIYA AWAMU YA SITA TRA
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kumekuwa na ongezeko la
ukusanyaji wa Mapato kutoka kwenye Halmashauri na kuwezesha maendeleo ndani ya
Mkoa pia kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania – Mkoa wa Dodoma.
kizungumza na Waandishi wa Habari leo Ofisi
kwake kupitia programu ya kutangaza Mafanikio ya Awamu ya Sita katika Kipindi
cha miaka miwili, Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma ulipangiwa Fedha za
miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani ambapo kumekuwa na ongezeko kutoka
shilingi 32,1 hadi kufikia shilingi 35.0 Sawa na 9%.
Mhe. Senyamule amesema ongezeko hili
limesaidia kuboresha huduma za jamii kwa kujenga vituo vya afya 4 zahanati 12
na vyumba vya madarasa 135 kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
“Tunaposema mapato yanaweza kuchangia
ongezeko la huduma kwa wananchi ni pamoja na sura hii ambayo imeonyesha ,Pia
mapato ya Halmashauri yanapoongezeka yameonyesha ongezeko la utoaji asilimia 10
kwa wananchi kwa makundi maalumu, Wanawake ,Vijana na Watu wenye ulemavu”
Alisisitiza Mhe. Senyamule
Amesema, Fedha za Mikopo ya wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu (Asilimia 10) zimeongezeka kutoka shilingi 4,68
hadi kufikia shilingi 5,58 sawa na 19%. Ongezeko hili limesaidia kuongezeka kwa
kiasi cha fedha kinachokopeshwa na idadi ya vikundi vinavyonufaika na mikopo
inayotolewa.
“Hii maana yake wananchi hawa wote
wataendelea kuongeza Mkopo ambao utawawezesha kuanzisha, kukuza na
kuongeza biashara ili kuwainua kiuchumi
kwa wananchi kwakuwa ndio lengo la Serikali kuwatengenezea wananchi mazingira
mazuri ,lakini fedha hizo pia za ongezeko katika Halmashauri zimewezesha
kupatikana kwa Shillingi millioni 250.8 ambazo zinatolewa kwa ajili ya
Watendaji wa kata 209 katika Mkoa wa Dodoma, Mpango ambao haujawahi kufanyika
katika awamu zote zilizopita” Senyamule alibainisha.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania Mkoa wa Dodoma, Sylver Rutagwelera ameelezea mafaniko
yaliopatika kwenye taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
Amesema katika kuhaikikisha Mamlaka ya
Mapato inapanua wigo wa walipakodi na kuongeza makusanyo ya kodi, Mamlaka ya
Mapato Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kusajili walipakodi wapya 12,076 kwa kipindi
cha Januari 2021 hadi Disemba 2022 kutokana na kuimarisha mahusiano mazuri kati
yake na walipakodi ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Lakini pia,Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Dodoma
imefanikiwa kusajili walipa kodi wapya 2,237 wanaotumia Mashine za kieletroniki
kwa mwaka 2022 pekee sambamba na hilo mkoa umeendelea kusimamia matumizi ya
mashine za EFD kwa kutoa elimu na pia kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria.
Hata hivyo, Mamlaka imefanikiwa kutoa elimu kwa walipa kodi na jamii kwa
ujumla ili kodi ilipwe bila shuruti na
matumizi ya nguvu yasio na lazima pia imekuwa ikisimamia na kudhibiti makusanyo
ya kodi.
Rutagwelera ameeleza katika kuhakikisha
wanaongeza makusanyo ya kodi mamlaka ya mapato Mkoa wa Dodoma imejipanga
kutekeleza ufatiliaji wa karibu wa matumizi ya mashine za EFD na ufatiliaji na
usajili wa wafanyabishara wapya kwenye kodi ya mapato na kodi ya ongezeko la
thamani.
Hata hivyo, ameelezea changamoto katika
ukusanyaji wa mapatao licha ya kutoa elimu ya kutosha imekuwa bado
wafanyabiashara na wananchi wamekuwa hawana elimu ya kutosha na ndio maana
wamekuwa wakitoa elimu hasa pembezoni mwa mji katika vijiji vya Chipogolo,
Mtera, Mbande, Songambele, Tubugwe, Hombolo, Mvumi misheni, Kibakwe, Wilaya ya
Bahi, Chemba, Chamwino na Kondoa.
Comments
Post a Comment