SENYEMULE AHIMIZA BALOZI KUJENGA DODOMA
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema mpaka sasa Balozi tatu (3) za
Uganda, Zimbambwe na Zambia zimeanza ujenzi wa majengo ya Balozi hizo Mkoani Dodoma.
Ameyasema
hayo leo tarehe 28/02/2023 mara baada ya kukutana na balozi wa Norway nchini
Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen aliembatana na ujumbe wake katika ziara ya kikazi
ya siku mbili ya kutembelea Mkoa wa Dodoma.
Mhe. Senyamule
amemshukuru Balozi wa Norway kwa kutembelea Dodoma, kuona fursa za uwekezaji na
kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili pia hatua mbalimbali
za utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika kuifaharisha Dodoma.
“Tunawakaribisha
sana Dodoma, makao makuu ya nchi yetu, viwanja 67 vimetengwa kwa ajili ya ujenzi
wa Ofisi na makazi ya balozi mbalimbali” Senyamule alisisitiza.
Ameongeza
kwa kusema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan ameendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi mikubwa ya
kimkakati ili Dodoma iweze kufunguka kimataifa.
Ameitaja
miradi hiyo kuwa ni pamoja ujenzi wa barabara za mzunguko, ndani na nje ya Mkoa
pamoja na ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato.
Naye Balozi wa Norway
nchini Tanzania Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen amesema kwa miaka mitano
aliyokaa Tanzania ameshuhudia mageuzi na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo
ambayo yamefanyika katika kipindi kifupi na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo agenda ya maendeleo endelevu.
Amesema kwa kipindi cha
miaka miwili Mkoa wa Dodoma umebadilika sana kutokana na uwekezaji uliofanyika
katika sekta ya miundombinu, Elimu, Afya na mazingira ya uwekezaji ikiwa ni
pamoja ujenzi wa mji wa Serikali.
Balozi Elisabeth katika
ziara yake ameambatana na ujumbe wa watu 21 na wanatembelea Mji wa Serikali Mtumba,
Hospitali ya Benjamin Mpaka, Ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa ndege wa Msalato.
Aidha, Mratibu wa kikosi
kazi cha Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe amesema ujio wa Balozi wa
Norway ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali kuhamia Dodoma hususani kuhamasisha
ujenzi wa ofisi za ubalozi na mashirika ya kitaifa.

Comments
Post a Comment