DODOMA YAJIPANGA KUINUA ELIMU










                                        

Idara ya Elimu Mkoa wa Dodoma imefikia maazimio kadhaa yenye lengo la kuinua sekta ya Elimu kwenye Mkoa wakati wa kikao kazi kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa Elimu chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule na Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Gugu kwenye ukumbi wa TAG - Mipango

Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na kuanzishwa kwa mfuko wa Elimu kwenye kila Halmashauri ili kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, utoaji wa chakula shuleni, kuthibiti utoro, hili, kila shule kuhakikisha kila mwanafunzi anamudu mada inayofundishwa, kila mwanafunzi anayemaliza Elimu ya Msingi anaanza masomo ya kujiandaa na kidato cha kwanza wiki mbili baada ya kufanya Mitihani.

Mhe. Senyamule amesema matarajio ya Serikali ya awamu ya sita ni kuona maendeleo makubwa kwenye sekta ya Elimu kutokana na uwekezajj Mkubwa uliofanyika kipindi hiki hivyo ni wajibu wa wadau wote wa Elimu, kukabiliana na changamoto zote zinazoikabili sekta hii.

"ikao hiki kimefuatia maagizo tuliyopeana ya kukaa vikao vya ngazi ya Vijiji, Kata, mpaka ngazi ya Wilaya ili kujadili namna ya kukabiliana na changamoto tunazoziona kwenye elimu. Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwenye elimu hivyo inatarajia kuona maendeleo mazuri kwenye elimu. Nitoe wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wadau, hakikisheni mnaongeza jitihada za kuthibiti utoro pia tuimarishe usimamizi katika ufundishaji kwa kutumia vitendea kazi ili kupandisha viwango vya ufaulu" Amesema Mhe. Senyamule

Naye, Katibu Tawala Mkoa Bw Ally Gugu, ameongelea malengo ya Kitaifa ya kuinua ufaulu kwenye Mitihani ya Taifa ambapo kwa kidato cha nne ni kutoka ufaulu wa asilimia 32 hadi kufikia asilimia 50 na kwa kidato cha sita ni kutoka asilimia 99.6 hadi asilimia 100. Pia amesisitiza juu ya wadau wa Elimu kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zote zinazoikabili sekta ya Elimu ili lengo kuu la Serikali kuinua sekta hii liweze kufikiwa hasa kwa Mkoa wa Dodoma.

Akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo kwa Mkoa, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Bw. Gift Kyando, amesema;

"Sekta ya Elimu bado inakabiliwa na changamoto za uchelewaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shuleni kwani lengo kuu la Mkoa ni kuinua ubora wa Elimu, utoro wa kudumu kwakuwa ni changamoto kwa shule, upungufu na uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa chakula, uwepo wa wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili, kuachia ajenda ya Elimu kwa Idara pekee na tatizo la jamii kulazimisha wanafunzi kujifelisha wakati wa Mitihani ya mwisho" Bw. Kyando. 

Kikao hiki kimebebwa na Kauli mbiu isemayo "Ubora wa Elimu ni jukumu letu sote: wadau tutimize wajibu wetu "

MWISHO

 

                          

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA