HUDUMA ZIENDANE NA UFANISI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefungua mafunzo ya wawezeshaji wa Mkoa na Wilaya (ToTs) wa Moduli ya Mfumo wa Mshitishi ('PVS IMPLEMENTATION MANUAL') pamoja na Mfumo wa kieletroniki wa mshitiri (PVIMIS)
Amefungua mafunzo hayo leo yatakayo fanyika kwa siku tatu yanayo ongozwa na wakufunzi Mfamasia Kirti Joshi na Bw. Haji Kisesa Afisa Tehama huku washiriki wakiwa ni Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Ally Gugu, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Best Magoma, Waganga Wakuu wa Wilaya Wafamasia, Watalaamu wa Maabara na Maafisa Tehama mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa uliopo jengo la Mkapa.
"Mtazamo wa
Serikali, nchi na dunia kwa ujumla unaenda kwenye Tehama kila kitu kinafanyika
kwa njia rahisi na kuondokana na mfumo wa Manual maana yake tunapopata njia ya
tehama maana yake tunaongeza ufanisi wa jambo tunalo lifanya kwaharaka, ubora,
muda mfupi kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikajii katika masuala ya fedha.
Nendeni mkafanyie kazi mfumo huu, Mjifunze kwa makini kwasababu ninyi mlio kuja ni ngazi ya wilaya ndio mnaosimamia vituo vya afya na Zahanati msiishie kufundisha wengine muwasimamie watumie vizuri huo mfumo ili ufanisi ulio kusudiwa na serikali uweze kuonekana ,ule mda mtakao pewa kwa ajili yakuanza kutumia mfumo sisi Mkoa wa Dodoma tunaharaka yakuanza kuutumia ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa madawa "Amesisitiza Mhe.Senyamule
Upande mwingine Mhe. Senyamule ametoa rai kwa watendaji hawa wanapoenda kufanya kazi na mshitiri kuondoa urasimu usio na sababu
Nae Bw. Edward
Magelewanya Mfamasia wa Mkoa ameishukuru TAMISEMI, Ofisi ya Katibu Tawala wa
Mkoa na serikali ya Uswiss (Swiss Hpss) kupitia mradi wa TUIMARISHE AFYA kwa
kuleta mfumo huu kwani utawasidia kuimarisha maboresho kwa huduma wanazotoa kwa
wananchi na kuboresha upatikaji wa bidhaa za afya.
Comments
Post a Comment