JIKITENI KWENYE KILIMO CHA UMWAGILIAJI MHE .SENYAMULE AWAASA WAKAZI WA KONDOA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Wilaya ya Kondoa kujikita katika kilimo Cha Umwagiliaji Ili kuondoa Janga la njaa, kujiongezea kipato na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ameyasema hayo leo tarehe 24/3/2023 kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kondoa ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi za Halmashauri, Ujenzi wa Hospitali ya Mji, Ujenzi wa Zahanati ya Ausia na kufanya Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Mnenia Wilaya ya Kondoa katika kiwanja cha Ofisi ya Kijiji Mnenia.
"Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita ameamua kuhimiza Kilimo cha umwagiliaji, kilimo cha uhakika ambacho mvua ikiisha unaendelea kumwagilia mpaka mazao yatakapo komaa. Kilimo ambacho maji yanakuwepo mwaka mzima unalima mara tatu au mara nne unavuna unalima tena na sisi mkoa wa Dodoma tumepata bahati kwa Wilaya tatu kuchimbiwa mabwawa na kuwekewa miundombinu ya umwagiliaji katika Wilaya za Mpwapwa, Chamwino na Bahi "Amesema Senyamule.
Aidha, Mhe. Senyamule ametoa rai na kusisitiza kutopandisha bei ya vyakula kwenye kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na mwezi Mtukufu wa Ramadhani
"Wale wanaofanya biashara ya chakula wakakikishe vyakula havipandi bei, wahakikishe wanauza chakula kwa bei ambayo hawaweki faida ya ziada kwasababu watu wapo kwenye Mfungo wa Ramadhani wanaongea na Mwenyezi Mungu wasipate adha nyingine tena ya kuwaza kuhusu kupanda kwa gharama za chakula, nitoe shime mkiona bei zinapanda bila sababu yeyote mtoe taarifa kwa viongozi wenu".
Upande mwingine Senyamule ametoa rai kwa wakandarasi wote wanao endelea na ujenzi wa miundombinu ya serikali kuhakikisha wanamaliza mradi hiyo kwa kuzingatia viwango vya ubora na kwa wakati kwa mujibu wa Mkataba.
Nae Mkuu wa Wilaya ya
kondoa Dkt. Khamis Mkanachi ametoa pongezi na Shukrani kwa ujio wa Mkuu wa Mkoa
kwa ziara yake kufanikiwa kusikiliza kero za wananchi wake na kufanikiwa kutoa
majibu ya changamoto za wananchi wa Kondoa.
Comments
Post a Comment