KILA KITU NI UTALI DODOMA MHE.ROSEMARY SENYAMULE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara ya Utalii wa Ndani siku mbili huku akiambatana na Wakuu wa Wilaya ya Chemba, Mpwapwa, Bahi, na Mwenyeji Kondoa katika Pori la Akiba Mkungunero
Lengo la ziara hiyo ni kuitangaza Mbuga ya Wanyama Mkungunero iliyopo wilaya ya kondoa yenye ukubwa kilomita za mraba 743 na urefu wa takribani kilomita 240 Kutoka Dodoma Mjini huku ikiwa na vivutio vingi ikiwa ni pamoja na wanyama wanne wakubwa kati ya watano. Mnyama anaekosekana katika pori hilo ni mmoja tu mnyama aina ya Faru.
Pori hili linajivunia kuwa na wanyama Tembo, Pofu, Punda-milia wanapatikana kwa wingi na Makundi makubwa Kiupekee mnyama Swalatwiga (Generac) katika eneo lote la Masai's Tepe anapatika katika eneo la Mkungunero tu na Tandara wa kubwa na wadogo ambacho ni kitu cha upekee sana ambacho ndicho kinawatambulisha.
"Tuendelee kuyaambia makundi mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma ambayo yamekuwa yakipenda kutembelea sehemu nyingine za hifadhi mfano wa Makundi Wanawake, vijana ambao hawajawahi kuja Mkungunero sasa nawaalika Makundi yaje na ntaendelea kuwa wakala mzuri wa Mbuga hii, wana Dodoma badala yakuenda sehemu nyingine tunatakiwa tuanzie nyumbani Makundi mengine kama Wizara, taasisi za dini ,vyuo, wafanya biashara na kila kundi katika sehemu zao za kupumzika waje Mkungunero" Amesema Mhe. Senyamule
Nae Kamanda wa Pori la Akiba Mkungunero Floravick Kalamba ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Royal Tour amefanikiwa kuleta watalii wengi ambao wanaleta fedha kwa ajili ya Tanzania .
"Tulifanikiwa kupata fedha ambazo zilifika kwa wakati sahihi ambapo Pori lilikuwa linahitaji kuwezeshwa katika miundombinu ya utalii, tulifanikiwa kujenga barabara ambazo zinapitika zenye urefu kwa kilomita 52 ,Tumejenga Lango la kupokea watalii ili kudhibiti ukusanyaji wa mapato, tumejenga jengo la kupumzikia watalii ambalo linaitwa pickin site"
Kamanda Kalamba
amewasihi wakazi wote wa Dodoma na Nje kwa ujumla kutembelea Pori hilo
kwani ni sehemu ambayo utaondoa msongo wa mawazo ya familia, kazi na
utajisikia tofauti baada kuingia ndani ya Pori la Akiba Mkungunero.
Comments
Post a Comment